“MBEGU
ZA UZIMA”
Tafakari
ya kila Jumapili
Jumapili,
Novemba 22, 2020
Dominika
ya 34 ya Mwaka
Sherehe
ya Yesu Kristo Mfalme
Eze
34:11-12.115-17
Zab
23:1-3.5-6
1Kor
15:20-26.28;
Mt
25:31-46
AGANO
JIPYA NA MFALME
Sherehe
ya Kristo Mlame ni sherehe ya Agano na Mungu. Mara nyingi tunavyosikia Agano
tunafikiria kuhusu Wayahudi walivyokuwa na Agano na Mungu. Lakini maanDiko
yanaitwa “Agano Jipya” na yanaonesha maagano yetu mapya na Bwana Mungu. Na
sehemu tulipofanya Agano hili ni siku ya Ubatizo. Tulibatizwa ndani ya Kristo
na ndani ya Agano jipya naye.
Somo
la kwanza linatoka katika kitabu cha nabii Ezekiel na linamuongelea Mungu kama
Mchungaji. “waliopotea nitawatafuta, waliopotea nitawarudisha, walio umia
nitawafunga majeraha….” Mara nyingi maneno makali katika Agano la Kale
yanawaogopesha watu siku hizi. Nabii Ezekieli akiongea kwa jina la Mungu
anatuambia “walio nona na wenye nguvu nitawangamiza”. Hii haina maana kwamba ni
Mungu anataka kuondoa na kuwaangamiza baadhi yetu. Bali ni kupigwa msasa na
Mungu nakutaka kumfanya mtu kuwa kiumbe kipya cha Kimungu. Wale wenye nguvu na
kunona mara nyingi huishi katika hali ya kujidanganya na kujiona watawala
lakini nguvu kamili ni Yesu. Hali ya kujidanganya inabidi iharibiwe au kupigwa
msasa na kurudishwa katika mstari wa kumfuata Yesu aliye mfalme wa kweli. Sisi
wote tunapaswa kujiweka kwake hakuna aliye mkuu zaidi. Tupo ndani ya Agano na
Mungu na Mfalme wetu ni Kristo.
Somo
la Pili linatoka katika barua ya kwanza ya Mtume Paulo kwa Wakorintho
inaongelea lengo kuu la kuishi katika maisha haya ni Kristo na kushiriki
ufufuko wake. Kila kitu kinapaswa kuwa kadiri ya mapenzi ya Mungu na kuishi
kadiri ya mapenzi hayo. Hivyo, kwanini tuna uhuru? Ili tuweze kujitoa wenyewe
kwa Kristo na kumfuata yeye daima. Mungu ana huruma sana juu yetu na hata
anatuvumilia kufanya kazi na sisi, hata kama hiyo kazi ni kwa ajili ya kutuunda
upya kwakuharibu yale yanayopinga mapenzi yake na kutupangia mipango mipya.
Katika
somo la Inili kutoka katika Injili ya Mathayo, anatuambia kwamba kadiri tunavyo
watendea hawa walio wadogo tunamtendea Kristo mwenyewe. Hili tunalifahamu kwa
akili zetu lakini mara nyingi hatulifanyi hili katika maisha yetu ya kila siku.
Tunapewa changamoto ya kumuona Yesu katika kila sura ya kila mtu, hasa wale
wanao tuudhi na kutufanyia kila lilolo baya na kujikuta sisi tunachukia kila
siku. Ndio maana Yesu anatuambia daima kwamba tuwapende maadui wetu. Ni rahisi
kumpenda rafiki.
Hadithi
moja ya Ireland, inaeleza wakati ambapo nchi ya Ireland ilitawaliwa na wafalme.
Mflame aliyekuwa anatawala hakuwa na mtoto wa kuirithi enzi yake. Hivyo,
aliwatuma wajumbe wake kutangaza ujumbe wake katika kila mji na kijiji cha
utawala wake. Aliwaalika vijana waliohitimu kwa mkutano na Mfalme. Mfalme
alihitaji sifa mbili: mtu lazima awe na upendo wa kina kwa Mungu na kwa jirani
yake.
Kijana
mmoja alisikia tangazo hilo. Kwa hakika alikuwa na upendo wa dhati wa Mungu na
kwa jirani. Lakini, alikuwa ni maskini sana, na hakuwa na mavazi ya adabu ya
kuvaa katika mkutano na hakuwa na fedha za kununulia mahitaji muhimu kwa ajili
ya safari ndefu kwenda kwenye ngome ya Mfalme. Aliamua kwenda kuomba nguo na
mahitaji aliyotaka. Kila kitu kilipokuwa tayari, alianza safari yake. Baada ya
mwezi mmoja wa safari, alifika karibu na ngome ya Mfalme, alimwona maskini
mwombaji akikaa kando ya barabara. Mwombaji alinyanyua mikono yake juu akiomba
msaada. “nina njaa na kujisikia baridi?” alisema kwa sauti ya kutetema, Je!
unaweza kunipa kitu chochote nipate kula na nguo kuvaa? Kijana yule alivutwa
sana na mwombaji. Alizitoa nguo zake za nje na kubadilishana na nguo za
mwombaji zilizochakaa na kuchanika. Pia alimpatia mwombaji yule mahitaji
aliyokuwa amebeba kwa ajili ya safari. Hii hairidhishi sana alitembea na nguo
zilizochakaa kwenda kwenye ngome ya Mfalme. Alipofika kwenye ngome ya Mfalme,
askari alimchukua kumpeleka eneo la wageni. Baada ya muda mrefu aliongozwa
kwenda kumwona Mfalme. Aliinama kifudifudi mbele ya enzi ya Mfalme na
aliponyanyua kichwa juu hakuweza kuamini macho yake. Alipomuona mfalme
alimwambia: “Wewe ulikuwa ni mwombaji kando ya barabara!” Hakika ni kweli”
alisema mfalme, “Nimetaka kujua zaidi kama hakika wampenda Mungu na jirani.”
Hadithi
hii hakika inalingana na liturujia ya leo. Mfalme wetu ni Mfalme mwenye Upendo.
Anatupenda sisi bila kikomo kwamba yeye alikuwa tayari kutoa utukufu wake
kutuokoa kutoka katika utumwa wetu wa dhambi. Ukweli alishuhudia Upendo. Je,
sisi tunaweza kusikiliza sauti ya upendo wake
Hivyo
kama Kristo Mfalme ni Mfalme wetu, tunapaswa kuishi agano letu naye. Tunapaswa
kutembea kwa unyenyekevu naye na kumwamini katika kuwapenda wenzetu na upendo
wa Mungu udhihirike katika maisha yetu. Sherehe hii sio tu kumwangalia Bwana
wetu kama Mfalme, hapana, nikutazama juu ya Agano letu na huyu Mfalme kama
tunatembea katika mapenzi ya Mfalme au tumechukua ule ufalme wake na kujifanya
sisi Wafalme? Yeye anataka kutupenda sisi daima kwasababu na sisi tunapenda
wote daima.
Tafakari
leo, juu ya kumpokea Kristo kama Mfalme. Je, yeye anaongoza maisha yako katika
kila nyanja? Je, unamruhusu yeye awe na uwezo wa kila kitu katika maisha yako?
Kama hili likifanyika kwa uhuru kamili ufalme wa Mungu unaanzishwa katika
maisha yako. Mwache yeye atawale ili wewe uweze kuongoka. Na kwa njia yako watu
waweze kumfahamu kama mfalme wa wote. Kama wajumbe wa Kristo Mfalme tutambue
kwamba sisi tutahukumiwa kwa njia ya sheria ya upendo pekee. Hivyo tujikabidhi
katika ufalme wake wa upendo.
Sala:
Bwana, wewe ni mfalme wa ulimwengu. Wewe ni Bwana wa wote. Njoo utawale maisha
yangu na ufanye moyo wangu kuwa sehemu yako ya kuishi. Bwana, njoo, ufanye
ulimwengu wetu kuwa sehemu yako ya amani na haki. Ufalme wako ufike! Yesu
nakuamini wewe. Amina.
Copyright
©2013-2020 ©FurKat, FurahayaKikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment