MASOMO
YA MISA, NOVEMBA 20, 2020
IJUMAA,
JUMA LA 33 LA MWAKA WA KANISA
SOMO
1
Ufu.
10:8 – 11
Mimi,
Yohane, nilisikia sauti ile niliyoisikia kutoka mbinguni ilinena nami tena,
ikisema, Enenda, ukakitwae kile kitabu kilichofunguliwa katika mkono wa yule
malaika, aliyesimama juu ya bahari na juu ya nchi. Nikamwendea malaika yule
nikamwambia kwamba anipe kile kitabu kidogo. Akaniambia, Kitwae, ukile, nacho
kitakutia uchungu tumboni mwako, bali katika kinywa chako kitakuwa kitamu kama
asali. Nikakitwaa kile kitabu kidogo katika mkono wa malaika yule, nikakila;
nacho kikawa kitamu kama asali kinywani mwangu, na nilipokwisha kukila tumbo
langu likatiwa uchungu. Wakaniambia, Imekupasa kutoa unabii tena juu ya watu na
taifa na lugha na wafalme wengi.
Neno
la Bwana… Tumshukuru Mungu.
WIMBO
WA KATIKATI
Zab.
119:14, 24, 72, 103, 111, 131 (K) 103
(K)
Mausia yako ni matamu sana kwangu.
Nimeifurahia
njia ya shuhuda zako,
Kana
kwamba ni mali mengi.
Shuhuda
zako ndizo furaha yangu,
Na
washauri wangu. (K)
Sheria
ya kinywa chako ni njema kwangu,
Kuliko
maelfu ya dhahabu na fedha.
Mausia
yako ni matamu sana kwangu,
Kupita
asalai kinywani mwangu. (K)
Shuhuda
zako nimezifanya urithi wa milele,
Maana
ndizo changamko la moyo wangu.
Nalifunua
kinywa changu nikatweta,
Maana
naliyatamani maagizo yako. (K)
SHANGILIO.
2Kor.
5:19
Aleluya,
aleluya,
Mungu
alikuwa ndani ya Kristu, akiupatanisha ulimwengu na nafsi yake, ametia ndani
yetu neno la upatanisho.
Aleluya.
INJILI
Lk.
19:45-48
Yesu
aliingia hekaluni, akaanza kuwatoa wale waliokuwa wakifanya biashara,
akiwaambia, Imeandikwa, Nyumba yangu itakuwa nyumba ya sala; lakini ninyi
mmeifanya kuwa pango la wanyang’anyi.
Naye
akawa akifundisha kila siku hekaluni. Lakini wakuu wa makuhani, na waandishi,
na wakuu wa watu walikuwa wakitafuta njia ya kumwangamiza; wasione la kutenda,
kwa kuwa watu wote walikuwa wakiandamana naye, wakimsikiliza.
Neno
la Bwana… Sifa kwako Ee Kristu.
-------------------------
Copyright
© 2020, "MASOMO YA MISA" published by T.M.P. Book Department, Tabora
– Tanzania. Readings reproduced by FurahayaKikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment