“ASALI
ITOKAYO MWAMBANI”
Ijumaa,
Novemba 20, 2020,
Juma
la 33 la Mwaka wa Kanisa
Mdo
28:11-16,30-31;
Zab
118:14,24,72,103,111,131;
Lk
19:45-48
KUSAFISHA
NA KUTAKASA HEKALU
Injili
ya leo inaongelea kuhusu kutakasa hekalu la Yerusalemu. Kwa Wayahudi, Hekalu
lilikuwa halina cha kufananisha nacho wala kulinganisha, kwasababu Mungu
mwenyewe amepachagua kukaa ndani yake.
Hekalu
la kwanza lililojengwa na Mfalme Solomoni mwaka 960 K.B. (1 Waf 6: 1)
liliharibiwa na Nebukadnezza mfalme wa Babuloni mwaka 587 K.B. (2 Mambo ya
Nyakati 36). Lilijengwa tena na Zerubabeli baada ya utumwa wa Babeli,
lilichafuliwa na Antikus Epifanes mfalme wa Seleucide mwaka 167 K.B.
Lilitakaswa tena mwaka 165 K.B na Yuda wa Makabayo na ndugu yake. Herodi ili
kupata heshima kutoka kwa Wayahudi aliliboresha na kulijenga vizuri hekalu hili
la pili na kujaribu kulirudisha katika hali ya utukufu wake wa mwanzo kazi
iliochukua miaka 46 (Yn 2: 20). Baada ya hekalu kubomolewa kabisa mpaka misingi
yake na Warumi mwaka 70 A.D, halikuwahi kujengwa tena. Katika eneo hilo kuna
msikiti wa Omar.
Yesu,
katika Injili ya leo analitakasa hekalu na anajaribu kulirudisha katika lengo
lake la mwanzo. Tunaisha katika nyakati zinazobadilika, kiasi kwamba kanisa
siku hizi baadhi ya watu wanaweza kuwa na malengo mengine.
1.Sehemu
ya Makumbusho- watu wanakuja kuona uzuri wa kanisa na rangi zake.
2.
Dukani- watu wanakuja kupata kitu kwa Mungu/kununua kitu kutoka kwa Mungu.
3.
Sehemu ya kulipa kodi-lazima nilipe fungu la kumi nisipolipa nitaadhibiwa mimi
na familia yangu.
4.
Sehemu ya Maonesho- sehemu ambayo watu wanakuja kujionesha, aina ya nguo, pete
yake mpya, mikufu, gari jipya, nguo mpya, na aina ya maisha ninayo ishi.
5.
Sehemu ya kuabudu-sehemu ambayo watu wanaweza kuhizi uwepo wa Mungu katika hali
ya nguvu kubwa tofauti na sehemu nyingine.
Mungu
ameamua kujidhihirisha katika hekalu, si kwa sababu hana sehemu nyingine-kwani
yeye ni Mkuu wa ulimwengu mzima. Ni sehemu iliowekwa wakfu ili kutusaidia
kujenga tena upya uhusiano wetu naye. Mzaburi anatuambia siku moja hekaluni mwa
Bwana ni bora kuliko siku elfu mahali pengine (Zab. 84:10). Je, wewe unaenda
kanisani kwa lengo ghani? Kuanzia namba moja hadi tano hapo juu wewe upo wapi?
Tujipime na kama tunakosea turudi katika lengo halisi la Hekalu.
Sala:
Bwana Yesu, nitakase mimi na uniweke tena katika hali ya neema na uaminifu.
Amina.
------------------------
Copyright
©2013-2020 ©FurKat, FurahayaKikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment