MASOMO
YA MISA, NOVEMBA 17, 2020
SOMO
1
Ufu.
3:1 – 6, 14 – 22
Mimi
Yohane, nilisikia Bwana anayeniambia: Kwa malaika wa kanisa lililoko Sardi
andika; Haya ndiyo anenayo yeye aliye na hizo Roho saba za Mungu, na zile nyota
saba. Nayajua matendo yako, ya kuwa una jina la kuwa hai, nawe umekufa. Uwe
mwenye kukesha, ukayaimarishe, ukayaimarishe mambo yaliyosalia, yanayotaka
kufa. Maana sikuona matendo yako kuwa yametimilika mbele za Mungu wangu.
Basi
kumbuka jinasi ulivyopokea, na jinsi ulivyosikia; yashike hayo na kutubu.
Walakini usipokesha, nitakuja kama mwivi, wala hutaijua saa nitakayokuja kwako.
Lakini unayo majina machache katika Sardi, watu wasioyatia mavazi yao uchafu.
Nao watakwenda pamoja nami hali wamevaa mavazi meupe, kwa kuwa wamestahili.
Yeye ashindaye atavikwa hivyo mavazi meupe, wala sitalifuta kamwe jina lake
katika kitabu cha uzima, nami nitalikiri jina lake mbele za Baba yangu, na
mbele ya malaika zake. Yeye aliye na sikio, na alisikie neno hili ambalo Roho
ayaambia makanisa.
Na
kwa malaika wa kanisa lililoko Laodikia andika; haya ndiyo anenayo yeye aliye
Amina, Sahahidi aliye mwaminifu na wa kweli, mwanzo wa kuumba kwa Mungu.
Nayajua matendo yako, ya kuwa hu baridi wala hu moto; ingekuwa heri kama
ungekuwa baridi au moto. Basi, kwa sababu una uvuguvugu, wala hu baridi wala
moto, nitakutapika utoke katika kinywa changu. Kwa kuwa wasema, Mimi ni tajiri,
nimejitajirisha, wala sina haja ya kitu; nawe hujui ya kuwa wewe u mnyonge, na
mwenye mashaka, na maskini, na kipofu, na uchi.
Nakupa
shauri, ununu kwangu dhahabu iliyosafishwa kwa moto, upate kuwa tajiri; na
mavazi meupe upate kuvaa, aibu ya uchi wako usionekane; na dawa ya macho ya
kujipaka macho yako, upate kuona. Wote niwapendao mimi nawakemea, na kuwarudi;
basi uwe na bidi, ukatubu. Tazama, nasimama mlangoni, nabisha; mtu akiisikia
sauti yangu, na kuufungua mlango, nitaingia kwake, nami nitakula pamoja naye,
na yeye pamoja nami.
Yeye
ashindaye, nitampa kuketi pamoja nami katika kiti changu cha enzi, kama mimi
nilivyoshinda nikaketi pamoja na Baba yangu katika kiti chake cha enzi. Yeye
aliye na sikio, na alisikie neno hili ambalo Roho ayaambia makanisa.
Neno
la Bwana… Tumshukuru Mungu.
WIMBO
WA KATIKATI
Zab.
15:1 – 4 (K) Ufu. 3:21
(K)
Yeye ashindaye, nitamketisha pamoja nami.
Bwana,
ni nani atakayekaa
Katika
hema yako?
Ni
mtu aendaye kwa ukamilifu,
Na
kutenda haki. (K)
Asemaye
kweli kwa moyo wake,
Asiyesingizia
kwa ulimi wake.
Wala
hakumtenda mwenziwe mabaya.
Wala
hakumsengenya jirani yake.
Machoni
pake mtu asiyefaa hudharauliwa,
Bali
huwaheshimu wamchao Bwana. (K)
Hakutoa
fedha yake apate kula riba,
Hakutwaa
rushwa amwangamize asiye na hatia.
Mtu
atendaye mambo hayo hataondoshwa milele. (K)
SHANGILIO
Lk.
8:15
Aleluya,
aleluya,
Wanabarikiwa
wale ambao kwa unyofu na wema wa mioyo yao, hulisikia neno la Mungu, na
kulishika.
Aleluya.
INJILI
Lk.
19:1-10
Yesu
alipoingia Yeriko alipita katikati yake. Na tazama, palikuwa na mtu, jina lake
Zakayo, mkubwa mmoja katika watoza ushuru, naye ni tajiri. Huyu alikuwa
akitafuta kumwona Yesu ni mtu wa namna gani, asiweze kwa sababu ya umati wa
watu, maana ni mfupi wa kimo. Akatangulia mbio, akapanda juu ya mkuyu apate
kumwona, kwa kuwa atakuja kuipitia njia ile.
Na
Yesu, alipofika mahali pale, alitazama juu, akamwambia, Zakayo, shuka upesi,
kwa kuwa leo imenipasa kushinda nyumbani mwako. Akafanya haraka, akashuka,
akamkaribisha kwa furaha. Hata watu walipoona, walinung’unika wote, wakisema,
Ameingia kukaa kwa mtu mwenye dhambi. Zakayo akasimama, akamwambia Bwana,
Tazama, Bwana, nusu ya mali yangu nawapa maskini, na ikiwa nimenyang’anya mtu
kitu kwa hila namrudishia mara nne. Yesu akamwambia, Leo wokovu umefika
nyumbani humu, kwa sababu huyu naye ni mwana wa Ibrahimu. Kwa kuwa Mwana wa
Adamu alikuja kutafuta na kuokoa kile kilichopotea.
Neno
la Bwana… Sifa kwako Ee Kristu.
-------------------------
Copyright
© 2020, "MASOMO YA MISA" published by T.M.P. Book Department, Tabora
– Tanzania. Readings reproduced by FurahayaKikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment