“ASALI
ITOKAYO MWAMBANI”
Tafakari
ya kila siku
Jumanne,
Novemba 17, 2020,
Juma
la 33 la Mwaka wa Kanisa
Ufu
3:1-6, 14-22;
Zab
14:2-5,
Lk
19:1-10
FURAHA
YA UPENDO WA YESU
Karibuni
ndugu zangu kwa tafakari ya neno la Mungu asubuhi ya leo. Leo kanisa linazidi
kutukumbusha juu ya ujio wa nyakati za mwisho na hivyo linatualika kumrudia
Mungu na kuwa na bidii zaidi.
Wimbo
wetu wa katikati unatueleza kwamba yule atakayeonesha bidii hii atapatiwa
nafasi ya kuushiriki utukufu mkuu utokao kwa Mwenyezi. Akina Musa, Elia na
Abrahamu ni miongoni mwa watu waliojitahidi na hivyo basi waliwezeshwa kukwea
mlima wa Bwana na kupewa utukufu na m
Mwenyezi
Mungu. Nasi tunahimizwa kuongeza bidii tuweze kuukuta utukufu huu.
Somo
letu la kwanza linaendeleza mada hii kwa undani zaidi. Katika ujumbe wake kwa
kanisa la Sardis, kanisa hili linaambiwa kwamba lilijiamini kupita kiasi kwamba
liko salama kumbe lina hali mbaya. Linaambiwa likazane liendeleze kile kidogo
kilichobaki nacho ili angalau lisipoteze kila kitu. Ujumbe huu unatuhusu na
sisi pia. Hata sisi tunayochembe ya imani na wema ambayo bado ipo ndani yetu
tuzidishe bidii angalau tuiwashe ili isizime kabisa. Hii ndio itakayotuokoa.
Hivyo
bidii na kuonyesha nia ni kitu kitakachomuokoa mkristo. Lakini uzembe na kukata
tamaa vitamuangusha. Sisi tuwe watu wa bidii. Pia katika ujumbe wake kwa kanisa
la Laodicea, linalaumiwa kwa sababu lilikuwa vuguvugu-lilikuwa na unafiki
mkubwa na lilichanganya mambo na kujiona liko salama kumbe liko kwenye hali
mbaya na hivyo linashauriwa lije na kununua dhahabu toka kwa Mwenyezi ili
litakaswe. Ni ujumbe tunaoambiwa na sisi ndugu zangu. Sisi ndio tunaochanganya
mambo. Tunakwenda kanisani na kwa waganga, tunavaa rozari na hirizi kwenye
mwili huu huu. Tunafanya uasherati tukiwa tumevaa hata rozari, tunalewa na bado
tunajiita wakristo. Kweli Mungu atatutapika. Twende kwake tuombe hii dhahabu
itutakase. Tuirudie sakramenti ya upatanisho nasi tutakuwa weupe tena.
Katika
injili, Zakayo anatuonyesha mfano wa kuja kununua hii dhahabu safi toka kwa
Yesu. Alipanda juu ili amuone na huu ukawa mwanzo wa uongofu wake kumfuata Yesu
na akatakaswa kabisa na hata kuanza kutubu.
Sisi
tuwe kama Zakayo, tupande juu na Yesu ataona bidii yetu na kuja kwetu.
Tunapanda juu kwa kuungama na Yesu atakuja kwetu sasa na kushiriki karamu
pamoja nasi kama iliyotokea kwa Zakayo. Ameni.
------------------------
Copyright
©2013-2020 ©FurKat, FurahayaKikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment