MASOMO YA MISA, NOVEMBA 14, 2020
JUMAMOSI,
JUMA LA 32 LA MWAKA
SOMO
1
3Yoh.
1:5 – 8
Mpenzi,
kazi ile ni ya uaminifu uwatendeayo hao ndugu na hao wageni nao, waliokushuhudia
upendo wako mbele ya kanisa; utafanya vizuri ukiwasafirisha kama ipasavyo kwa
Mungu. Kwa maana, kwa ajili ya Jina hilo, walitoka, wasipokee kitu kwa Mataifa.
Basi imetupasa sisi kuwakaribisha watu kama hao, ili tuwe watenda kazi pamoja
na kweli.
Neno
la Bwana… Tumshukuru Mungu.
WIMBO
WA KATIKATI
Zab.
112:1 – 6 (K) 1
(K)
Heri mtu yule amchaye Bwana.
Aleluya.
Heri
mtu yule amchaye Bwana,
Apendezwaye
sana na maagizo yake
Wazao
wake watakuwa hodari duniani;
Kizazi
cha wenye adili kitabarikiwa. (K)
Nyumbani
mwake mna utajiri na mali,
Na
haki yake yakaa milele.
Nuru
huwazukia wenye adili gizani;
Ana
fadhili na huruma na haki. (K)
Heri
atendaye fadhili na kukopesha;
Atengenezaye
mambo yake kwa haki.
Kwa
maana hataondoshwa kamwe;
Mwenye
haki atakumbukwa milele. (K)
SHANGILIO
Zab.
130:5
Aleluya,
aleluya,
Roho
yangu inamngoja Bwana, na neno lake nimelitumainia.
Aleluya.
INJILI
Lk.
18:1-8
Yesu
aliwaambia wanafunzi wake mfano, ya kwamba imewapasa kumwomba Mungu sikuzote,
wala wasikate tamaa. Akasema, Palikuwa na kadhi katika mji Fulani, hamchi
Mungu, wala hajali watu. Na katika mji huo palikuwa na mwanamke mjane,
aliyekuwa akimwendea-endea, akisema, Nipatie haki na adui wangu. Naye kwa muda
alikataa; halafu akasema moyoni mwake, Ijapokuwa simchi Mungu wala sijali watu,
lakini, kwa kuwa mjane huyu ananiudhi, nitampatia haki yake, asije akanichosha
kwa kunijia daima.
Bwana
akasema, Sikilizeni asemavyo yule kadhi dhalimu. Na Mungu, je! Hatawapatia haki
wateule wake wanaomlilia mchana na usiku, naye ni mvumilivu kwao? Nawaambia,
atawapatia haki upesi; walakini, atakapokuja Mwana wa Adamu, je! Ataiona Imani
duniani?
Neno
la Bwana… Sifa kwako Ee Kristu.
-------------------------
Copyright
© 2020, "MASOMO YA MISA" published by T.M.P. Book Department, Tabora
– Tanzania. Readings reproduced by FurahayaKikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment