“ASALI
ITOKAYO MWAMBANI”
Tafakari
ya kila siku
Jumamosi,
Novemba 14, 2020,
Juma
la 32 la Mwaka wa Kanisa
3Yn
1:5-8;
Zab
111:1-6;
Lk
18:1-8
KUVUMMILIA
KATIKA SALA!
Karibuni
ndugu zangu kwa adhimisho la Misa takatifu asubuhi ya leo. Leo tafakari yetu
inaanza kwa kuliangalia somo la kwanza ambapo tunakutana na Yohane akiwahimiza
waamini kuwapokea wamisionari na viongozi wao wa dini. Wasiwaache wahangaike au
kunyanyaswa na wapagani bali wawe baba na mma kwao.
Ilikuwa
rahisi kwa wamisionari kunyanyaswa kwa sababu waliishi mbali na nyumbani na kwa
kiasi kikubwa walitegemea misaada. Hivyo kama watakutana na Wakristo
wasiowakarimu, moja kwa moja waliishia hata kuangukia mikononi mwa wapagani
ambao waliwanyanyasa. Wakristo wa mwanzo waliwajali sana wamisionari wao
kuepuka wasinyanyaswe na wapagani.
Hili
nasi tuliige leo.Tusiwatupe wamisionari wetu, mapadre, masista,
makatekista-tusiwatupe. Hawa hufanya kazi mbali na nyumbani mwao. Tunapaswa
kuwa baba na mama kwao. Tukiwaacha watanyanyaswa na wapagani, watakwenda
kufanya biashara huko na wapagani watawanyanyasa hata kuwafunga gerezani.
Tusikubali hili. Tusikubali waangukie mikononi mwa wapagani-tusikubali
wanyanyaswe na wapagani. Tuwatunze kama kaka na wadogo zetu, wajisikie nyumbani
kabisa. Tusikubali ardhi wanayoitunza kwa ajili ya kanisa inyanganywe toka kwao
hivihivi na watu wapagani. Tuwatee. Tusikubali kabisa waonewe. Tuwalishe
wamisionari wetu kwa kuwa wakarimu kwao ili waendeleze kazi ya Kristo vyema.
Katika
injili, Yesu anahimiza tusikate tamaa, tuombe bila kuchoka, kuomba inahitaji
unyenyekevu, ni wale tu wenye unyenyekevu wanaofanikiwa. Wengi wetu tunashindwa
kuomba kwa sababu ya kutokujishusha na tunataka tupate haraka.
Tusije
na roho ya namna hii mbele ya Mungu kila tuendapo kwa maombi mbele ya Mungu.
Mungu anahuruma kubwa kuliko huyu kadhi. Kama kadhi aliweza kumpatia huyu mama
haki yake, hakika Mungu atatupatia na sisi haki zetu tena kwa ziada kubwa
kabisa. Nasi tuwe tayari kuwapatia wenzetu haki zao.
Tusizungushezungushe
watu. Tuwapatie iliyohaki yao na wajapo kwetu mara kwa mara, tusionyeshe ugumu
wa moyo-tufungue mioyo yetu na kuwapatia haki yao. Tusikubali kuwa sababu ya
kilio kwa wengine. Wapo waliodhulumiwa ardhi, nyumba na mali mbali mbali ambao
daima hutokwa na machozi, hakika Mungu atawasikia na anayedhulumu hatabaki
salama kwani huwezi kupigana na Mungu.
------------------------
Copyright
©2013-2020 ©FurKat, FurahayaKikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment