MASOMO YA MISA, NOVEMBA 13, 2020
IJUMAA,
JUMA LA 32 LA MWAKA WA KANISA
SOMO
1
2Yoh.
1:4 – 9
Nalifurahi
mno kwa kuwa nimewaona baadhi ya watoto wako wanaenenda katika kweli, kama vile
tulivyopokea amri kwa Baba. Na sasa, mama, nakuomba, si kwamba nakuandikia amri
mpya, bali ile tuliyokuwa nayo tangu mwanzo, kwamba tupendane.
Na
huu ndio upendo; tuenende kwa kuzifuata amri zake. Hii ndiyo ile amri, kama
mlivyosikia tangu mwanzo kwamba mwenende katika hiyo.
Kwa
maana wadanganyifu wengi wametokea duniani, wasiokiri ya kuwa Yesu Kristo yuaja
katika mwili. Huyo ndiye yule mdanganyifu na mpinga Kristo. Jiangalieni nafsi
zenu msiyapoteze mliyoyatenda, bali mpokee thawabu timilifu. Kila apitaye cheo,
wala asidumu katika mafundisho ya Kristo, yeye hana Mungu. Yeye adumuye katika
mafundisho hayo, huyo ana Baba na Mwana pia.
Neno
la Bwana… Tumshukuru Mungu.
WIMBO
WA KATIKATI
Zab.
119:1 – 2, 10 – 11, 17 – 18 (K) 1
(K)
Heri waendao katika sheria ya Bwana.
Heri
walio kamili njia zao,
Waendao
katika sheria ya Bwana.
Heri
wazitiio shuhuda zake,
Wamtafutao
kwa moyo wote. (K)
Kwa
moyo wangu wote nimekutafuta,
Usiniache
nipotee mbali na maagizo yako.
Moyoni
mwangu nimeliweka neno lako,
Nisije
nikakutenda dhambi. (K)
Umtendee
mtumishi wako ukarimu,
Nipate
kuishi, nami nitalitii neno lako.
Unifumbue
macho yangu niyatazame
Maajabu
yatokayo katika sheria yako. (K)
SHANGILIO
Zab.
119:28, 33
Aleluya,
aleluya,
Unitie
nguvu sawasawa na neno lako, Ee Bwana, unifundishe njia ya amri zako.
Aleluya.
INJILI
Lk.
17:26-37
Yesu
aliwaambia wanafunzi wake: Na kama ilivyokuwa siku za Nuhu, ndivyo itakavyokuwa
katika siku zake Mwana wa Adamu. Walikuwa wakila na kunywa, walikuwa wakioa na
kuolewa, hata siku ile Nuhu aliyoingia katika safina, gharika ikashuka
ikawaangamiza wote. Na kadhalika, kama ilivyokuwa katika siku za Lutu, walikuwa
wakila na kunywa, walikuwa wakinunua na kuuza, wakipanda na kujenga; lakini
siku ile Lutu aliyotoka Sodoma kulikunya moto na kibiriti kutoka mbinguni
vikawaangamiza wote. Hivyo ndivyo itakavyokuwa siku ile atakayofunuliwa Mwana
wa Adamu.
Katika
siku ile, aliye juu ya dari, na vyombo vyake vimo ndani ya nyumba, asishuke ili
kuvitwaa; na kadhalika, aliye shambani asirejee nyuma. Mkumbukeni mkewe Lutu.
Mtu yeyote atakaye kuiponya nafsi yake, ataiangamiza; na yeyote
atakayeiangamiza ataiponya. Nawaambia, usiku huo watu wawili watakuwa katika
kitanda kimoja; mmoja atatwaliwa, mmoja ataachwa. Wanawake wawili watakuwa
wakisaga pamoja; mmoja atatwaliwa, mmoja ataachwa.
Wakajibu,
wakamwuliza, Wapi, Bwana? Akawaambia. Ulipo mzoga, ndipo watakapokutanika tai.
Neno
la Bwana… Sifa kwako Ee Kristu.
-------------------------
Copyright
© 2020, "MASOMO YA MISA" published by T.M.P. Book Department, Tabora
– Tanzania. Readings reproduced by FurahayaKikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment