“ASALI ITOKAYO MWAMBANI”
Tafakari
ya kila siku
Ijumaa,
Novemba 13, 2020,
Juma
la 32 la Mwaka wa Kanisa
2Yn
1:4-9
Zab
118:1-2, 10-11, 17-18
Lk
17:26-37
KUJIWEKA
TAYARI KWA UPENDO!
Karibuni
ndugu zangu kwa adhimisho la Misa Takatifu asubuhi ya leo. Leo tafakari yetu
inaongozwa na zaburi yetu ya wimbo wa katikati inayosisitizia kwamba wana heri
wale waitiio sheria ya Bwana. Umuhimu wa sheria hii ni kumfundisha mtu hekima.
Na kweli utashangaa, wale wanaokazana kuitambua sheria ya Bwana huishia kuwa na
moyo wa hekima mara nyingi hata zaidi ya wale walio hata na kisomo kikubwa.
Utashangaa
kuona maandishi ya baadhi ya watakatifu ambao waliyaandika katika sala.
Mafundisho yao huvutia zaidi kuliko yale ya wenye elimu ya kidunia. Hata
wahubiri wanaosali kabla ya kuhubiri huishia kutoa mahubiri mazuri zaidi. Kweli
sheria ya Bwana humfunza mjinga hekima na kumtii Bwana ni chanzo cha hekima
hii. Tumtii Bwana nasi tutapata hekima. Ndio maana utashangaa kuona kwamba
wengi wanapendelea kesi zao ziamuliwe na viongozi wao wa dini kuliko na
mahakimu waliopo mitaani. Sheria ya Bwana humfundisha mtu hekima.
Huu
ujumbe wa zaburi unasisitizia vyema ujumbe wa Yohane katika somo la kwanza
kwamba ni wale tu wanao yatii mafundisho ya Bwana wanaweza kuwa na Roho wa
Bwana. Manabii wa uongo wanakosa utii ndio maana wanamkosa Roho wa Bwana. Sisi
tuwe watii na wanyenyekevu zaidi, tuikumbatie sheria ya Bwana na hakika
tutakuwa na hekima zaidi. Maisha yetu yamekosa mvuto kwa wengi kwa sababu ya
ukosefu wa utii kwa Bwana. Tuzidishe uchaji kwa Bwana nasi tutakuwa na hekima
na mvuto kama wana wa Mungu.
Yesu
katika Injili anasema siku za mwisho wana wa dunia hii bado watakuwa wanaonesha
mizaha mizaha tu na kutokujiandaa kama walivyomfanyia Nuhu. Aliijenga safina
kwa miaka 120 lakini hakuna aliyebadilika hadi ile siku ya gharika na watu
kuangamia.
Sisi
tuache mizaha kwa mambo ya Mungu. Mambo ya Mungu tunayafanyia mno maigizo.
Wengine tunayatumia kufichia uovu wetu. Kama tumeamua kubadilika tuanze kweli.
Mizaha na ukosefu wa maamuzi sahihi yanatuangusha kwa kiasi kikubwa sana. Na
Yesu amedhihirisha kwamba kutakuwa na uchaguzi-mnaweza kuwa wawili mahali
pamoja lakini mmoja atatwaliwa na mwingine aachwa. Wale wenye mizaha mizaha
ndio watakao achwa na wengine kutwaliwa. Tuache mizaha hii ndugu zangu. na
tusiyaone mambo matakatifu kama maigizo. Tuache kufanya maigizo na mambo
matakatifu. Wengi tumezidisha maigizo na mambo haya. Tusiyatumie kufichia uovu
wetu.
------------------------
Copyright
©2013-2020 ©FurKat, FurahayaKikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment