ASALI
ITOKAYO MWAMBANI”
tafakari
ya kila siku
Alhamisi,
Novemba 19, 2020,
Juma
la 33 la Mwaka wa Kanisa
Ufu
5:1-10;
Zab
149:1-6, 9;
Lk
19:41-44
JE,
TUNAPATA UTUKUFU KATIKA YERUSALEMU YA ZAMANI AU KATIKA YERUSALEMU MPYA?
Karibuni
ndugu zangu kwa tafakari ya neno la Mungu asubuhi ya leo katika adhimisho la
Misa Takatifu. Leo wimbo wetu wa katikati ni wa shukrani ukimshukuru Mungu kwa
kutufanya kuwa wanaukoo wakifalme na kikuhani tuweze kumtumikia yeye. Ndio
sababu za kufurahi katika wimbo wetu wa katikati.
Katika
somo letu la kwanza, tunagundua kwamba aliyetutendea haya ni Yesu mwenyewe kwa
sababu yeye hakuogopa au kuona aibu au kufa moyo. Alikubali kuchinjwa na kwa
damu yake akaweza kutununua. Na kama asingalifanya hivi, hakika angalikosekana
wa kukifungua kitabu au chuo kinachozungumziwa leo katika somo letu la kwanza.
Kitabu hiki kilikuwa cha muhimu kwani ndicho kilichobeba ujumbe kuhusu mpango
wa Mungu juu ya ulimwengu. Na kweli kama Yesu asingalikuwa mtii hakika
asingalitokea wa kuweza kukitwaa hicho kitabu na kikifungua.
Sisi
ndugu zangu tunahitajika tukakifungue kitabu, Mungu anapenda kututumia kufungua
kitabu na hivyo basi lazima tuwe na utii na tuepukane na majivuno. Halafu ni
lazima tuwe watu wa sadaka zaidi, tusikatishwe tamaa kirahisi tuvumilie. Hivi
vilimsaidia Yesu. Sisi tuache uvivu; ukitukanwa au kujibiwa vibaya tu
usilalamike kana kwamba ni mtu kakuua. Bado songa mbele.
Katika
injili, Yesu anaeleza hasara ziwapatazo wale walio na kiburi. Yerusalemu
ilikuwa hivyo. Ilitawaliwa na watu waliojiona kuwa wanaweza kila kitu
wakifikiri kwamba umaarufu wa mji utawaokoa; sio hivyo.
Yesu
anawaambia kwamba mtashangaa mtakapoona kwamba mji wenu wote unaangushwa.
Somo
hili linatuhusu sisi tulio na kiburi. Wengi tunafikiri kwamba akili zetu
zitatuokoa, au kitendo cha kuwa kiongozi kanisani, labda mwenyekiti wa
halimashauri ya walei au uongozi mwingine, au mwenyekiti wa chama cha kitume
ndio inakuwa tayari nimeshaokoka, au kwa kitendo cha kushinda kanisani
nimeshaokoka. Hapana. Wokovu hupatikana katika bidii na unyenyekevu. Lazima
tuwe watu wa kufanya bidii, tujione kuwa hatustahahili. Hapa ndio tutashinda.
Tukifikiri
ati tutashinda kwa hela au akili au kwasababu nina kazi nzuri serikalini au kwa
nguvu zetu kamwe hatutaweza kusonga popote. Tukiwa na mali au uwezo wa kiakili
alafu tukakosa unyoofu tunapoteza ladha kabisa. Tupambwe na unyenyekevu Yesu
atatusifu.Tumsifu Yesu Kristo.
------------------------
Copyright
©2013-2020 ©FurKat, FurahayaKikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment