“ASALI ITOKAYO MWAMBANI”
Tafakari ya kila siku
Jumapili, Oktoba 25, 2020
Juma la 30 la Mwaka
Kut 22:20-26;
Zab 17:2-4, 47, 51;
1Thes 1:5-10;
Mt 22:34-40
UPENDO:ALAMA YA UFUASI WA
KIKRISTO!
Masomo ya leo yanatualika
tutafakari juu ya msingi wa maisha ya kila mfuasi wa Kristo yalipojengwa:
upendo kwa Mungu na jirani. Wakati mwingine tunapotezwa katika mawazo mabaya
kuhusu upendo kwa Mungu na kwa jirani. Ni vizuri kutafakari juu ya hili mara
kwa mara. Mwalimu wa Sheria alimuuliza Yesu swali ili kumtega. “ni Amri ipi
iliyo kuu zaidi katika sheria?’ Ni wazi uhusiano wa Yesu na hawa viongozi wa
dini unaonekana ulikuwa una malumbano. Walikuwa wakimjaribu hata kumtega.
Lakini kama kawaida Yesu aliendelea kuwanyamazisha kwa maneno yake ya hekima.
Yesu alimjibu mwalimu wa
sheria kwamba “umpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote kwa akili zako zote…
“hii ni amri kubwa kuliko zote na ya pili, “mpende jirani yako kama nafsi yako”
(Mt 22:37-39). Yesu anatoa ufupisho wa sheria zote za maadili zinazo patikana
katika Amri kumi za Mungu. Amri tatu za mwanzo, zinasisitiza upendo kwa Mungu
kwa moyo wote. Na amri nyingine zinasisitiza upendo kwa jirani. Sheria ya
maadili ya Mungu ni rahisi kama hizi amri mbili tu zinavyosema.
Mfuasi wa Kristo anapaswa
kufuata sheria ya upendo. Sheria hii ina nyanja mbili –upendo kwa Mungu na
upendo kwa jirani, na hii inakuwa ni alama ya ufuasi wetu. Nini maana ya
kumpenda Mungu na jirani? Kwanza kabisa upendo wa Mungu ni kuuelewa upendo wa
Mungu kwetu sisi. Sisi ni dhaifu kabisa na hatuwezi kumpenda Mungu kama
inavyopaswa. Lakini kwa njia ya Kristo tunaweza kufahamu kwamba Mungu
anatupenda. Hivyo kufahamu upendo wa Mungu licha ya kwamba mtu ni dhaifu
inamfanya mtu ampende Mungu kama shukrani. Na huu ndio mwanzo wa upendo. Wakati
mtoto mdogo anavyofahamu upendo wa mama juu yake, hauleti chochote kwa Mama.
Huu ndio upendo wetu kwa Mungu. Wakati tunavyo ufahamu upendo wa Mungu sisi
hatuongezi chochote kwa Mungu, hatuta anguka kwenye dhambi tutafana na yale
yanayo mpendeza yeye. Inamfurahisha Mungu tunavyo pendana sisi kwa sisi. Mmoja
akianza kumpenda Mungu, anaanza pia kuwapenda wengine.
Somo la kwanza leo kutoka
katika kitabu cha kutoka linaelezea amri ya Mungu kwa wana wa Israeli: upendo
kwa jirani. Ni wakati gani upendo wangu kwa jirani utakuwa mkamilifu? Tunapo
wapenda majirani zetu tunatamani na wao wapate nafasi katika ufalme wa Mungu.
Tunakuwa tunatamani kama wataishi katika neema ya Mungu siku zote za maisha
yao. Na hivyo waweze kuishi milele kwa sababu ya neema tuliopokea kutoka kwa
Kristo. Tukiwapenda wenzetu namna hii hatuwezi kuwanyima chochote au mahitaji
yeyote wanayo taka kwetu. Tunakumbuka alichosema Yesu, kwamba mlicho watendea
wadogo hawa mlinitendea mimi. Tunaenda kuwatembelea watu walio katika mahitaji
mbali mbali kwa njia ambazo zipo katika uwezo wetu. Na huu ndio upendo kwa
jirani.
Mt. Paulo katika barua
yake kwa Wathesalonike katika somo la pili leo, anawakumbusha umuhimu wa
kuongoka katika Imani ya maisha ya Kikristo, ambapo ni kumtumikia Mungu na
kumtumikia Mwanae Yesu Kristo aliye mfunua Baba na Roho kwetu.
Tafakari juu ya wito wa
kumpenda Mungu na jirani kwa jinsi ulivyo. Fikiria juu ya neno “wote” kupenda
kwa moyo “wote”, na ukitafakari kuhusu hili utatambua njia ambazo umeshindwa
kutoa kitu kwa ajili ya Mungu na hata kwa jirani. Ukiona upungufu wako, anza
tena kwa kujikabidhi katika kuwa zawadi kwa Mungu na kwa jirani.
Sala: Bwana, ninachagua
kukupenda wewe kwa Moyo wangu wote, akili na utashi wote na nguvu. Nipe neema
niweze kuishi amri hizi mbili za upendo na kuziona kama njia za kuelekea kwenye
utakatifu wa maisha. Ninakupenda Bwana wangu. Yesu nakuamini wewe. Amina
Copyright ©2013-2020
©FurKat, FurahayaKikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment