MASOMO YA MISA,
OKTOBA
25, 2020
DOMINIKA
YA 30 YA MWAKA
MWANZO:
Zab.
105:3-4
Ufurahi
moyo wao wamtafutao Bwana. Mtakeni Bwana na nguvu zake, utafuteni uso wake siku
zote.
SOMO
1
Kut.
22:21-27
Usimwonee
mgeni, wala kumtendea jeuri; kwa kuwa ninyi mlikuwa wageni katika nchi ya
Misri. Usimtese mjane yoyote aliyefiwa na mumewe, wala mtoto yatima. Ukiwatesa
watu hao katika neno lolote, nao wakanililia mimi, hakika yangu nitasikia kilio
chao, na hasira yangu itawaka moto, nami nitawaua ninyi kwa upanga; na wake
wenu watakuwa wajane, na watoto wenu mayatima. Ukimkopesha mtu aliye maskini,
katika watu wangu walio pamoja nawe; usiwe kwake mfano wa mwenye kumdai; wala
hutamwandikia faida. Ikiwa wewe kwa njia yoyote wapokea nguo ya jirani yako
rehani, lazima utamrudishia mbele ya jua kuchwa; maana hiyo nguo ni kifuniko
chake, hiyo peke yake ni nguo ya ngozi yake; je! Atalalia nini? Itakuwa, hapo
atakaponililia mimi, nitasikia; kwa kuwa mimi ni mwenye rehema.
Neno
la Bwana… Tumshukuru Mungu.
WIMBO
WA KATIKATI
Zab.
18:1-3, 46, 50 (K) 1
(K)
Wewe, Bwana, nguvu yangu, nakupenda sana.
Wewe
Bwana, nguvu zangu, nakupenda sana;
Bwana
ni jabali langu, na boma langu,
Na
mwokozi wangu. (K)
Mungu
wangu, mwamba wangu ninayemkimbilia,
Ngao
yangu, na pembe ya wokovu wangu,
Na
ngome yangu.
Nitamwita
Bwana astahiliye kusifiwa,
Hivyo
nitaokoka na adui zangu. (K)
Bwana
ndiye aliye hai,
Na
atukuzwe Mungu wa wokovu wangu.
Ampa
mfalme wokovu mkuu.
Amfanyia
fadhili masihi wake. (K)
SOMO
2
1Thes.
1:5-10
Kama
vile mnavyojua jinsi zilivyokuwa tabia zetu kwenu, kwa ajili yenu. Nanyi mkawa
wafuasi wetu na wa Bwana, mkiisha kulipokea neno katika dhiki nyingi, pamoja na
furaha ya Roho Mtakatifu. Hata mkawa kielelezo kwa watu wote waaminio katika
Makedonia, na katika Akaya. Maana kutoka kwenu neno la Mungu limevuma, si
katika Makedonia na Akaya tu, ila na kila mahali imani yenu mliyo nayo kwa
Mungu imeenea; hata hatuna haja sisi kunena lolote. Kwa kuwa wao wenyewe
wanatangaza habari zetu, jinsi kulivyokuwa kuingia kwetu kwenu; na jinsi
mlivyomgeukia Mungu mkaziacha sanamu, ili kumtumikia Mungu aliye hai, wa kweli;
na kumngojea Mwanae kutoka mbinguni, ambaye alimfufua katika wafu, naye ni
Yesu, mwenye kutuokoa na ghadhabu itakayokuja.
Neno
la Bwana… Tumshukuru Mungu.
SHANGILIO
Yn.
1:12, 14
Aleluya,
aleluya,
Naye
neno alifanyika mwili, akakaa kwetu; Wote waliompokea aliwapa uwezo wa
kufanyika watoto wa Mungu.
Aleluya.
INJILI
Mt.
22:34-40
Mafarisayo
waliposikia ya kwamba amewafumba kinywa wale Masadukayo, walifanya shauri
pamoja. Mmoja wao, mwanasheria, akamwuliza, akimjaribu; Mwalimu, katika torati
ni amri ipi iliyo kuu? Akamwambia, Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote,
na kwa roho yako yote, na kwa akili zako zote. Hii ndiyo amri iliyo kuu, tena
ni ya kwanza. Na ya pili yafanana nayo, nayo ni hii, Mpende jirani yako kama
nafsi yako. Katika amri hizi mbili hutegemea torati yote na manabii.
Neno
la Bwana… Sifa kwako Ee Kristu.
________
-------------------------
Copyright
© 2020, "MASOMO YA MISA" published by T.M.P. Book Department, Tabora
– Tanzania. Readings reproduced by FurahayaKikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment