MASOMO
YA MISA OKTOBA 28, 2020
JUMATANO
JUMA LA 30 LA MWAKA
SIKUKUU
YA WATAKATIFU SIMONI NA YUDA, MITUME
SOMO
1
Efe.
2:19-22
Tangu
sasa ninyi si wageni wala wapitaji, bali ninyi ni wenyeji pamoja na watakatifu,
watu wa nyumbani mwake Mungu. Mmejengwa juu ya msingi wa mitume na manabii,
naye Kristo Yesu mwenyewe ni jiwe kuu la pembeni. Katika yeye jengo lote
linaungamanishwa vema na kuku ahata liwe hekalu takatifu katika Bwana. Katika
yeye ninyi nanyi mnajengwa pamoja kuwa maskani ya Mungu katika Roho.
Neno
la Bwana… Tumshukuru Mungu.
WIMBO
WA KATIKATI
Zab.
19:1-4 (K) 4
(K)
Sauti yao imeenea duniani mwote.
Mbingu
zauhubiri utukufu wa Mungu,
Na
anga laitangaza kazi ya mikono yake.
Mchana
husemezana na mchana,
Usiku
hutolea usiku maarifa. (K)
Hakuna
lugha wala maneno,
Sauti
yao haisikilikani.
Sauti
yao imeenea duniani mwote,
Na
maneno yao hata miisho ya ulimwengu.
Katika
hizo ameliwekea jua hema. (K)
SHANGILIO
Aleluya,
aleluya,
Ee
Mungu, tunakusifu, tunakukiri kuwa Bwana. Jamii tukufu ya Mitume inakusifu.
Aleluya.
INJILI
Lk.
6:12-16
Yesu
aliondoka akaenda mlimani ili kuomba, akakesha usiku kucha katika kumwomba
Mungu. Hata kulipokuwa mchana aliwaita wanafunzi wake; akachagua kumi na wawili
miongoni mwao, ambao aliwaita Mitume; Simoni, aliyemwita jina la pili Petro, na
Andrea nduguye, na Yakobo na Yohane, na Filipo na Bartolomayo, na Mathayo na
Tomaso, na Yakobo wa Alfayo, na Simoni aitwaye Zelote, na Yuda wa Yakobo, na
Yuda Iskariote, ndiye aliyekuwa msaliti.
Neno
la Bwana… Sifa kwako Ee Kristu.
-------------------------
Copyright
© 2020, "MASOMO YA MISA" published by T.M.P. Book Department, Tabora
– Tanzania. Readings reproduced by FurahayaKikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment