MASOMO YA MISA, OKTOBA 26,
2020
JUMATATU, JUMA LA 30 LA
MWAKA
SOMO 1
Efe. 4:32 – 5:8
Iweni wafadhili ninyi kwa
ninyi, wenye huruma mkasameheane kama na Mungu katika Kristo alivyowasamehe ninyi.
Hivyo mfuateni Mungu,
kama watoto wanaopendwa; mkaenende katika upendo, kama Kristo naye
alivyowapenda ninyi; tena akajitoa kwa ajili yetu, sadaka na dhabihu kwa Mungu,
kuwa harufu ya manukato. Lakini uasherati usitajwe kwenu kamwe, wala uchafu
wowote wala kutamani, kama iwastahilivyo watakatifu; wala aibu wala maneno ya
upuzi wala ubishi; hayo hayapendezi; bali afadhali kushukuru. Maana neno hili
mnalijua hakika, ya kwamba hakuna mwasherati wala mchafu wala mwenye tamaa,
ndiye mwabudu sanamu, aliye na urithi katika ufalme wa Kristo na Mungu.
Mtu asiwadanganye kwa
maneno yasiyo na maana; kwa kuwa kwa sababu ya hayo hasira ya Mungu huwajia
wana wa uasi. Basi msishirikiane nao. Kwa maana zamani ninyi mlikuwa giza, bali
sasa mmekuwa nuru katika Bwana; enendeni kama watoto wa nuru.
Neno la Bwana… Tumshukuru
Mungu.
WIMBO WA KATIKATI
Zab. 68:1, 3, 5 – 6, 19 –
20 (K)
(K) Mfuateni Mungu, kama
watoto wanaopendwa.
Heri mtu yule asiyekwenda
Katika shauri la wasio
haki; wala hakusimama katika njia ya wakosaji;
Wala hakuketi barazani pa
wenye mizaha.
Bali sheria ya Bwana
ndiyo impendezayo,
Na sheria yake
huitafakari mchana na usiku. (K)
Naye atakuwa kama mti
uliopandwa
Kandokando ya vijito vya
maji,
Uzaao matunda yake kwa
majira yake,
Wala jani lake halinyauki;
Na kila alitendalo
litafanikiwa. (K)
Sivyo walivyo wasio haki;
Hao ni kama makapi
yapeperushwayo na upepo,
Kwa kuwa Bwana anaijua
njia ya wenye haki.
Bali njia ya wasio haki
itapotea. (K)
SHANGILIO
Yak. 1:18
Aleluya, aleluya,
Kwa kupenda kwake
mwenyewe, Baba alituzaa sisi kwa neno la kweli, tuwe kama limbuko la viumbe
vyake.
Aleluya.
INJILI
Lk. 13:10-17
Siku ya sabato Yesu
alikuwa akifundisha katika sinagogi mojawapo. Na tazama, palikuwa na mwanamke
aliyekuwa na pepo wa udhaifu muda wa miaka kumi na minane, naye amepindana,
hawezi kujinyosha kabisa. Yesu alipomwona alimwita, akamwambia, Mama,
umefunguliwa katika udhaifu wako. Akaweka mikono yake juu yake, naye akanyoka
mara hiyo, akamtukuza Mungu.
Basi mkuu wa sinagogi
alikasirika kwa sababu Yesu amemponya mtu siku ya sabato, akajibu akawaambia
mkutano, Kuna siku sita zifaazo kufanya kazi, basi njoni mponywe katika siku
hizo, wala si katika siku ya sabato. Lakini Bwana akamjibu akasema, Enyi
wanafiki, kila mmoja wenu, Je! Hamfungi ng’ombe wake au punda wake siku ya
sabato katika zizi, aende naye kumnywesha? Na huyu mwanamke, aliye wa uzao wa
Ibrahimu, ambaye Shetani amemfunga miaka kumi na minane hii, haikupasa
afunguliwe kifungo hiki siku ya sabato? Aliposema haya wakatahayari wote walioshindana
naye; mkutano wote wakafurahi kwa sababu ya mambo matukufu yaliyotendwa na
yeye.
Neno la Bwana… Sifa kwako
Ee Kristu.
-------------------------
Copyright
© 2020, "MASOMO YA MISA" published by T.M.P. Book Department, Tabora
– Tanzania. Readings reproduced by FurahayaKikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment