ASALI
ITOKAYO MWAMBANI”
Tafakari
ya kila siku
Jumatatu,
Oktoba 26, 2020,
Juma
la 30 la Mwaka wa Kanisa
Ef
4:32 – 5:8;
Zab
1:1-4, 6;
Lk
13:10-17
HURUMA
YA MUNGU!
Karibuni
ndugu zangu kwa tafakari ya neno la Mungu katika adhimisho la Misa Takatifu
asubuhi ya leo. Leo tafakari yetu inaanza kwa kuliangalia somo la kwanza ambapo
miongoni mwa msisitizo ni Paulo kuwaambia wakristo wa Efeso kwamba waishi vyema
na wawe na kauli njema toka kinywani mwao, maneno machafu yasisikie kamwe
mdomoni mwao. Maneno yao yawe ya kutia moyo na yenye kuponya matatizo ya watu
na si kuwakatisha tamaa.
Ndugu
zangu, maneno mabaya naya kudharau yamewaumiza wengi; wengi wamepata magonjwa
na kujeruhiwa vibaya kwa sababu ya maneno mabaya. Kinyume chake ni kwamba
maneno mazuri yameweza kuwa uponyaji kwa wengi. Sisi ndugu zangu kama wakristo
maneno na majibu yetu lazima yawe ya kutia moyo kwa yeyote. Huu ndio ukarimu
tunaoweza kuwaonyesha watu hata kama ikitokea hatuna pesa za kuwapa watu. Kauli
nzuri ndio ukarimu wetu na msaada wetu kwa watu. Kauli yangu nzuri inatosha.
Kingine
pia ni kutumia vinywa vyetu vyema kwenye kuongea maneno mazuri. Wengi wetu hasa
vijana tunatumia muda mwingi kuongea habari zisizofaa; kinywa chetu
kinamtangaza shetani zaidi kuliko Mungu. Tubadilike. Tusiache shetani atamalaki
zaidi ndani ya vinywa vyetu; akitawale kama chake.
Katika
injili, tunakutana na mama akiponywa leo na baada ya kuponywa anamtukuza Mungu.
Cha ajabu ni kwamba anapoponywa na kuanza kumtukuza tu Mungu, mkuu wa sinagogi
anakasirika. Yeye anashindwa kuangalia lile jambo zuri kwamba Mungu ametukuzwa
bali anaishia kukasirika na kusema sheria ya sabato imevunjwa.
Ndivyo
tulivyo kwa wengi wetu. Mara nyingi tukitenda jambo, tunakasumba ya kuangalia
hasi kuliko chanya. Huu ni ugonjwa wa wengi wetu. Jamani kuna na upande chanya
na tuombe tuwe watu wa kuona upande chanya pia. Tumehukumu wengi kwa sababu ya
kuangalia upande mmoja tu. Tufungue macho jamani. Kuna pande mbili pia na
ziangalie zote pia. Wengi tumeshindwa kuishi na wenzetu, na kugombana nao kila
siku kwa sababu ya kuangalia upande mmoja tu. Hatujui kwamba kuna pande mbili
pia tunazopaswa kuziangalia. Ebu tufungue macho zaidi na kuangalia pande zote
mbili kama maisha yetu hayatabadiliika na kuwa tofauti kabisa na uhusiano wetu
na watu kubadilika.
------------------------
Copyright
©2013-2020 ©FurKat, FurahayaKikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment