MASOMO
YA MISA OKTOBA 24, 2020
JUMAMOSI,
JUMA LA 29 LA MWAKA
SOMO
1
Efe.
4:7 – 16
Kila
mmoja wetu alipewa neema kwa kadiri ya kipimo cha kipawa chake Kristo. Hivyo
husema, Alipopaa juu aliteka mateka, Akawapa wanadamu vipawa.
Basi
neno hilo, Aliopaa, maana yake nini kama siyo kusema kwamba yeye naye alishuka
mpaka pande zilizo chini, za nchi? Naye aliyeshuka ndiye yeye aliyepaa; juu
sana kupita mbingu zote, ili avijaze vitu vyote. Naye alitoa wengine kuwa
mitume; na wengine kuwa manabii; na wengine kuwa wainjilisti; na wengine kuwa
wachungaji na waalimu; kwa kusudi la kuwakamilisha watakatifu, hata kazi ya
huduma itendeke, hata mwili wa Kristo ujengwe; hata na sisi sote tutakapoufikia
umoja wa Imani na kumfahamu sansa Mwana wa Mungu, hata kuwa mtu mkamilifu, hata
kufika kwenye cheo cha kimo cha utimilifu wa Kristo.
Tusiwe
tena watoto wachanga, tukitupwa huku na huku, na kuchukuliwa na kila upepo wa
elimu, kwa hila ya watu, kwa ujanja, tukizifuata njia za udanganyifu. Lakini
tuishike kweli katika upendo na kuku ahata tumfikie yeye katika yote, yeye
aliye kichwa, Kristo. Katika yeye mwili wote ukiungamanishwa na kushikanishwa
kwa msaada wa kila kiungo, kwa kadiri ya utendaji wa kila sehemu moja moja,
huukuza mwili upate kujijenga wenyewe katika upendo.
Neno
la Bwana… Tumshukuru Mungu.
WIMBO
WA KATIKATI
Zab.
122:1 – 5 (K) 1
(K)
Nalifurahi waliponiambia, na twende nyumbani kwa Bwana.
Nalifurahi
waliponiambia,
Na
twende nyumbani kwa Bwana.
Miguu
yetu imesimama
Ndani
ya malango yako, Ee Yerusalemu. (K)
Ee
Yerusalmeu uliyejengwa
Kama
mji ulioshikamana,
Huko
ndiko waliopanda kabila,
Kabila
za Bwana. (K)
Ushuhuda
kwa Israeli,
Walishukuru
jina la Bwana.
Maana
huko viliwekwa viti vya hukumu,
Viti
vya enzi vya mbari ya Daudi. (K)
SHANGILIO
2Tim.
1:10
Aleluya,
aleluya,
Mwokozi
wetu Yesu Kristo alibatili mauti, na kuufunua uzima na kutokuharibika kwa
Injili.
Aleluya.
INJILI
Lk.
13:1-9
Wakati
huo walikuwapo watu waliompasha Yesu habari ya Wagalilaya wale ambao Pilato
alichanganya damu yao na dhabihu zao. Akawajibu akwaambia, Je! Mwadhani ya
kwamba Wagalilaya hao walikuwa wenye dhambi kuliko Wagalilaya wote, hata
wakapatwa na mambo hayo? Nawaambia, Sivyo; lakini msipotubu, ninyi nyote
mtaangamia vivyo hivyo. Au wale kumi na wanane, walioangukiwa na mnara huko
Siloamu, ukawaua mwadhani ya kwamba wao walikuwa wakosaji kuliko watu wote
waliokaa Yerusalemu? Nawaambia, Sivyo; lakini msipotubu, ninyi nyote mtaangamia
vivyo hivyo.
Akanena
mfano huu; Mtu mmoja alikuwa na mtini umepandwa katika shamba lake la mizabibu;
akaenda akitafua matunda juu yake, asipate. Akamwambia mtunzaji wa shamba la
mizabibu, Tazama, miaka mitatu hii naja nikitafuta matunda juu ya mtini huu,
nisipate kitu; uukate, mbona hata nchi unaiharibu? Akajibu akamwambia, Bwana,
uuache mwaka huu nao, hata niupalilie, niutilie samadi; nao ukizaa matunda baadaye,
vema! La, usipozaa, ndipo uukate.
Neno
la Bwana… Sifa kwako Ee Kristu.
-------------------------
Copyright
© 2020, "MASOMO YA MISA" published by T.M.P. Book Department, Tabora
– Tanzania. Readings reproduced by FurahayaKikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment