MASOMO
YA MISA, OKTOBA 22, 2020
ALHAMISI,
JUMA LA 29 LA MWAKA
SOMO
1
Efe.
3:14 – 21
Nampigia
Baba magoti, ambaye kwa jina lake ubaba wote wa mbinguni na wa duniani unaitwa,
awajalieni, kwa kadiri ya utajiri wa utukufu wake, kufanywa imara kwa nguvu,
kwa kazi ya Roho wake, katika utu wa ndani.
Kristo
akae mioyoni mwenu kwa Imani mkiwa na shina na msingi katika upendo; ili mpate
kufahamu pamoja na watakatifu wote jinsi ulivyo upana, na urefu, na kimo, na
kina; na kuujua upendo wake Kristo, upitao ufahamu kwa jinsi ulivyo mwingi,
mpate kutimilika kwa utimilifu ulivyo mwingi, mpate kutimilika kwa utimilifu
wote wa Mungu.
Basi
atukuzwe yeye awezaye kufanya mambo ya ajabu mno kuliko yote tuyaombayo au
tuyawazayo, kwa kadiri ya nguvu itendayo kazi ndani yetu, naam, atukuzwe katika
Kanisa na katika Kristo Yesu hata vizazi vyote vya milele na milele. Amina.
Neno
la Bwana… Tumshukuru Mungu.
WIMBO
WA KATIKATI
Zab.
33:1 – 2, 4 – 5, 11 – 12, 18 – 19 (K) 5
(K)
Nchi imejaa fadhili za Bwana.
Mpigieni
Bwana vigelegele, enyi wenye haki,
Kusifu
kunawapasa wanyofu wa moyo.
Mshukuruni
Bwana kwa kinubi,
Kwa
kinanda cha nyuzi kumi mwimbieni sifa. (K)
Kwa
kauwa neno la Bwana lina adili,
Na
kazi yake yote huitenda kwa uaminifu.
Huzipenda
haki na hukumu,
Nchi
imejaa fadhili za Bwana. (K)
Shauri
la Bwana lasimama milele,
Makusudi
ya moyo wake vizazi na vizazi.
Heri
taifa ambalo Bwana ni Mungu wao,
Watu
aliowachagua kuwa urithi wake. (K)
Tazama,
jicho la Bwana li kwao wamchao,
Wazingojeao
fadhili zake.
Yeye
huwaponya nafsi zao na mauti,
Na
kuwahuisha wakati wa njaa. (K)
SHANGILIO
Yn.
17: 17
Aleluya,
aleluya,
Neno
lako ndiyo kweli, Ee Bwana, ututakase kwa ile kweli.
Aleluya.
INJILI
Lk.
12:49-53
Yesu
aliwaambia wanafunzi wake: Nimekuja kutupa moto duniani; na ukiwa umekwisha
washwa, ni nini nitakalo zaidi? Lakini nina ubatizo unipasao kubatiziwa, nami
nina dhiki kama nini hata utimizwe!
Je!
Mwadhani ya kwamba nimekuja kuleta amani duniani? Nawaambia, La, sivyo, bali
mafarakano. Kwa kuwa tokea sasa katiak nyumba moja watakuwamo watu watano
wamefarakana, watatu kwa wawili, wawili kwa watatu. Watafarakana baba na
mwanawe, na mwana na babaye; mama na binti yake, nab inti na mamaye; mkwe na
mtu na mkwewe, mkwe na mkwe mtu.
Neno
la Bwana… Sifa kwako Ee Kristu.
-------------------------
Copyright
© 2020, "MASOMO YA MISA" published by T.M.P. Book Department, Tabora
– Tanzania. Readings reproduced by FurahayaKikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment