MASOMO
YA MISA, OKTOBA 20, 2020
JUMANNE,
JUMA LA 29 LA MWAKA
SOMO
1
Efe.
2:12 – 22
Msisahau
kwamba zamani zile mlikuwa hamna Kristo, mmefarakana na jamii ya Israeli,
wageni wasio wa maagano ya ahadi ile. Mlikuwa hamna tumaini, hamna Mungu
duniani. Lakini sasa, katika Kristo Yesu, ninyi mliokuwa mbali hapo kwanza
mmekuwa karibu kwa damu yake Kristo. Kwa maana yeye ndiye amani yetu,
aliyetufanya sisi sote tuliokuwa wawili kuwa mmoja; akakibomoa kiambaza cha
kati kilichotutenga. Naye akiisha kuuondoa ule uadui kwa mwili wake; ndiyo
sheria ya amri zilizo katika maagizo; ili afanye hao wawili kuwa mtu mpya mmoja
ndani ya nafsi yake; akafanya amani. Akawapatanisha wote wawili na Mungu katika
mwili mmoja, kwa njia ya msalaba, akiisha kuufisha ule uadui kwa huo msalaba.
Akaja akahubiri amani kwenu ninyi mliokuwa mbali, na amani kwao wale waliokuwa
karibu. Kwa maana kwa yeye sisi sote tumepata njia ya kumkaribia Baba katika
Roho mmoja.
Basi
tangu sasa ninyi si wageni wala wapitaji, bali ninyi ni wenyeji pamoja na
watakatifu, watu wa nyumbani mwake Mungu. Mmejengwa juu ya msingi wa mitume na
manabii, naye Kristo Yesu mwenyewe na jiwe kuu la pembeni. Katika yeye jingo
lote linaungamanishwa vema na kuku ahata liwe hekalu takatifu katika Bwana.
Katika ninyi nanyi mnajengwa pamoja kuwa maskani ya Mungu katika Roho.
Neno
la Bwana… Tumshukuru Mungu.
WIMBO
WA KATIKATI
Zab.
85:9 – 14 (K) 9
(K)
Bwana anawaambia watu wake amani.
Nisikie
atakavyosema Bwana,
Maana
atawaambia watu wake amani.
Hakika
wokovu wake u karibu na wamchao,
Utukufu
ukae katika nchi yetu. (K)
Fadhili
na kweli zimekutana,
Haki
na amani zimebusiana.
Kweli
imechipuka katika nchi,
Haki
imechungulia kutoka mbinguni. (K)
Bwana
atatoa kilicho chema,
Na
nchi yetu itatoa mazao yake.
Haki
itakwenda mbele zake,
Nayo
itazifanya hatua zake kuwa njia. (K)
SHANGILIO
Yn.
10:27
Aleluya,
aleluya,
Kondoo
wangu waisikia sauti yangu, nami nawajua, nao wanifuata.
Aleluya.
INJILI
Lk. 12:35-38
Yesu
aliwaambia wanafunzi wake: Viuno vyenu na viwe vimefungwa, na taa zenu ziwe
zinawaka; nanyi iweni kama watu wanaomngojea bwana wao, atakaporudi kutoka
arusini, ili atakapokuja na kubisha, wamfungulie mara. Heri watumwa wale, ambao
bwana wao ajapo atawakuta wanakesha. Amin, nawaambieni, atajifunga na
kuwakaribisha chakulani, atakuja na kuwahudumia. Na akija zamu ya pili, au
akija zamu ya tatu, na kuwakuta hivi, heri watumwa hao.
Neno
la Bwana… Sifa kwako Ee Kristu.
-------------------------
Copyright
© 2020, "MASOMO YA MISA" published by T.M.P. Book Department, Tabora
– Tanzania. Readings reproduced by FurahayaKikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment