“ASALI
ITOKAYO MWAMBANI”
Tafakari
ya kila siku
Jumanne,
Oktoba 20, 2020
Juma
la 29 la Mwaka
Efe
2:12-22
Zab
85: 9-14;
Lk
12: 35-38.
KUWA
MWEPESI KUMKARIBISHA YESU
Karibuni
ndugu zangu kwa tafakari ya neno la Bwana katika adhimisho la Misa Takatifu
asubuhi ya leo. Leo basi tunaanza kwa kuiangalia zaburi yetu ya wimbo wa
katikati ambapo tunamkuta Mwenyezi Mungu akiwatakia amani watu wake.
Paulo
katika somo la kwanza anaendeleza msemo huu wa amani kwa kusisitiza ukweli
kwamba amani ya kweli imeletwa na Kristo mwenyewe. Ndiye aliyeteseka na kufuta uadui
uliokuwa baina ya mwanadamu na Mungu na hata baina ya wanadamu na wanadamu.
Amekomesha uadui uliokuwa kati ya Wayahudi na watu wa mataifa na kuwafanya kuwa
kitu kimoja. Ndiyo maana tukikutana kama wakristo, lugha yetu lazima iwe ya
Kristo-makabila, rangi, kisomo, urefu au ufupi vyote huisha. Lugha yetu hubakia
kuwa moja yaani ya Kristo.
Lakini
kwa bahati mbaya tumeshindwa katika hili. Bado tunashuhudia wabatizwa wakiishi
katika uadui mkubwa-wakati mwingine makabila yameonekana kuwa ya maana zaidi
kuliko hata ukristo wetu. Tumeshuhudia wakristo wakifanyiana visa vikubwa na
wengine kuuana bila kujali kwamba mwenzake ni mbatizwa. Yote haya ni ukiukwaji
wa ukristo wetu na imani yetu.
Tumeshuhudia
wakristo hata wakitengana-tumekubali kuona wenzetu wanakufa njaa mbele ya macho
yetu na sisi hatufanyi kitu na bado tunajiita Wakristo. Lazima tubadilike
tuishi ukristo wetu. Umoja unaoletwa na Kristo utatusaidia sana zaidi ya ule
umoja tunaofikiri utaletwa na makabila, rangi, lugha au tabaka letu. Tukimkumbatia
Kristo tutafaidi zaidi. Tumkumbatie Kristo.
Huku
ndiko kukesha kunakoelezewa katika injili ya leo. Yesu anataka akija atukute
tuko kama watumishi wanaowatumikia wenzao na kweli akija atatupa tuzo. Lakini
akitukuta katika hali ya kutengana na kunyanyasana kwa makabila au watu wa
tabaka za chini. Akitukuta katika ubinafsi wa kuwanyonya wengine kana kwamba
hao sio binadamu au katika hali ya kutokujali-hakika atatuadhibu vibaya sana.
Kukesha
ni kuwatumikia wenzetu. Tumsifu Yesu Kristo.
------------------------
Copyright
©2013-2020 ©FurKat, FurahayaKikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment