MASOMO
YA MISA, OKTOBA 19, 2020
JUMATATU,
JUMA LA 29 LA MWAKA
SOMO
1
Efe.
2:1 – 10
Mlikuwa
wafu kwa sababu ya makosa na dhambi zenu; ambazo mliziendea zamani kwa kuifuata
kawaida ya ulimwengu huu, na kwa kumfuata mfalme wa uwezo wa anga, roho yule
atendaye zake sasa katika wana wa kuasi; ambao zamani, sisi sote nasi
tulienenda kati yao, katika tamaa za miili yetu, tulipoyatimiza mapenzi ya
mwili nay a nia, tukawa kwa tabia yenu watoto wa hasira kama na hao wengine.
Lakini Mungu, kw akuwa ni mwingi wa rehema, kwa mapenzi yake makuu
aliyotupenda; hata wakati ule tulipokuwa wafu kwa sababu ya makosa yetu;
alituhuisha pamoja na Kristo; yaani mmeokolewa kwa neema. Akatufufua pamoja
naye, akatuketisha pamoja naye katika ulimwengu war oho, katika Kristo Yesu.
Ili
katika zamani zinazokuja audhihirishe wingi wa neema yake upitao kiasi kwa wema
wake kwetu sisi katika Kristo Yesu. Kwa maana mmeokolewa kwa neema, kwa njia ya
Imani; ambayo hiyo haikutokana na nafsi zenu, ni kipawa cha Mungu; wala si kwa
matendo, mtu awaye yote asije akajisifu. Maana tu kazi yake, tuliumbwa katika
Kristo Yesu, tutende matendo mema, ambayo tokea awali Mungu aliyatengeneza ili
tuenende nayo.
Neno
la Bwana… Tumshukuru Mungu.
WIMBO
WA KATIKATI
Zab.
100 (K) 3
(K)
Ndiye aliyetuumba, na sisi tu watu wake.
Mfanyieni
Bwana shangwe, dunia yote;
Mtumikieni
Bwana kwa furaha;
Njoni
mbele zake kwa kuimba. (K)
Jueni
kwamba Bwana ndiye Mungu;
Ndiye
aliyetuumba na sisi tu watu wake;
Tu
watu wake, na kondoo wa malisho yake. (K)
Ingieni
malangoni mwake kwa kushukuru;
Nyuani
mwake kwa kusifu;
Mshukuruni,
lihimidini jina lake. (K)
Kwa
kuwa Bwana ndiye mwema;
Rehema
zake ni za milele;
Na
uaminifu wake vizazi na vizazi. (K)
SHANGILIO
Yn.
8:12
Aleluya,
aleluya,
Mimi
ndimi nuru ya ulimwengu, asema Bwana, yeye anifuataye hatakwenda gizani kamwe,
bali atakuwa na nuru ya uzima.
Aleluya.
INJILI
Lk.
12;13-21
Mtu
mmoja katika mkutano alimwambia Yesu, Mwalimu, mwambie ndugu yangu anigawie
urithi wetu. Akamwambia, Mtu wewe, ni nani aliyeniweka mimi kuwa mwamuzi au
mgawanyi juu yenu? Akawaambia, Angalieni, jilindeni na choyo, maana uzima wa
mtu haumo katika wingi wa vitu vyake alivyo navyo.
Akawaambia
mithali, akisema, Shamba la mtu mmoja tajiri lilikuwa limezaa sana; akaanza
kuwaza moyoni mwake, akisema, Nifanyeje? Maana sina pa kuyaweka akiba mavuno
yangu. Akasema, Nitafanya hivi; nitazivunja ghala zangu, nijenge nyingine kubwa
zaidi, na humo nitaweka nafaka yangu yote na vitu vyangu. Kisha, nitajiambia,
Ee nafsi yangu, una vitu vyema vingi ulivyojiwekea akiba kwa miaka mingi;
pumzika basi, ule, unywe, ufurahi. Lakini Mungu akamwambia, Mpumbavu wewe,
usiku huu wa leo wanataka roho yako! Na vitu ulivyojiwekea tayari vitakuwa vya
nani? Ndivyo alivyo mtu ajiwekeaye nafsi yake akiba, asijitajirishe kwa Mungu.
Neno
la Bwana… Sifa kwako Ee Kristu.
-------------------------
Copyright
© 2020, "MASOMO YA MISA" published by T.M.P. Book Department, Tabora
– Tanzania. Readings reproduced by FurahayaKikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment