MASOMO
YA MISA, OCTOBA 31, 2020
JUMAMOSI,
JUMA LA 30 LA MWAKA
SOMO
1
Flp.
1:18 – 26
Kristo
anahubiriwa; na kwa hiyo nafurahi, naam, nami nitafurahi. Maana najua ya kuwa
haya yatanigeukia kuwa wokovu wangu, kwa sababu ya kuomba kwenu, na kuruzukiwa
Roho wa Yesu Kristo; kama vile nilivyotazamia sana, na kutumaini, kwamba
sitaaibika kamwe, bali kwa uthabiti wote, kama siku zote, na sasa vivyo hivyo
Kristo ataadhimishwa katika mwili wangu; ikiwa kwa maisha yangu, au ikiwa kwa
mauti yangu.
Kwa
maana kwangu mimi kuishi ni Kristo, na kufa ni faida. Ila ikiwa kuishi katika
mwili, kwangu mimi ni matunda ya kazi; basi nitakalolichagua silitambui.
Ninasongwa katikati ya mambo mawili; ninatamani kwenda zangu nikae na Kristo;
maana ni vizuri zaidi sana; bali kudumu katika mwili kwahitajiwa zaidi kwa
ajili yenu. Nami nikitumaini hayo, najua ya kuwa nitakaa na kudumu pamoja
nanyi, ili mpate kuendelea na kufurahi katika Imani; hata mzidi kuona fahari
katika Kirso Yesu juu yangu kwa sababu ya kuwapo kwangu pamoja nanyi tena.
Neno
la Bwana… Tumshukuru Mungu.
WIMBO
WA KATIKATI
Zab.
42:1 – 2, 4 (K) 2
(K)
Nafsi yangu inamwonea kiu Mungu.
Kama
ayala aioneavyo shauku mito ya maji.
Vivyo
hivyo nafsi yangu inakuonea shauku, Ee Mungu. (K)
Nafsi
yangu inamwonea kiu Mungu, Mungu aliye hai,
Lini
nitakapokuja nionekane mbele za Mungu? (K)
Jinsi
nilivyokuwa nikienda na mkutano,
Na
kuwaongoza nyumbani kwa Mungu,
Kwa
sauti ya furaha na kusifu. (K)
SHANGILIO
Zab.
19:8
Aleluya,
aleluya,
Amri
ya Bwana ni safi, huyatia macho nuru.
Aleluya.
INJILI
Lk.
14:1, 7-11
Yesu
alipoingia ndani ya nyumba ya mtu mmoja miongoni mwa wakuu wa Mafarisayo siku
ya sabato, ale chakula, walikuwa wakimvizia.
Akawaambia
mfano wale walioalikwa, alipoona jinsi walivyochagua viti vya mbele; akisema,
Ukialikwa na mtu arusini, usiketi katika kiti cha mbele; isiwe kwamba amealikwa
mtu mwenye kustahiwa kuliko wewe, akaja yule aliyewaalika wewe na yeye, na
kukuambia, Mpishe huyu! Ndipo utakapoanza kwa haya kushika mahali pa nyuma, ili
ajapo yule aliyekualika akuambie, Rafiki yangu, njoo huku mbele Zaidi; ndipo
utakapokuwa na utukufu mbele ya wote walioketi pamoja nawe. Kwa maana kila
ajikwezaye atadhiliwa, naye ajidhiliye atakwezwa.
Neno
la Bwana… Sifa kwako Ee Kristu.
-------------------------
Copyright
© 2020, "MASOMO YA MISA" published by T.M.P. Book Department, Tabora
– Tanzania. Readings reproduced by FurahayaKikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment