“ASALI
ITOKAYO MWAMBANI”
Tafakari
ya kila siku
Jumamosi,
Octoba 30 , 2020,
Juma
la 30 la Mwaka wa Kanisa
Flp
1: 18-26;
Zab
42: 2-3, 5;
Lk
14: 1, 7-11
KUWA
WA KWANZA!
Karibuni
ndugu zangu kwa tafakari ya neno la Bwana asubuhi ya leo katika adhimisho la
Misa Takatifu. Zaburi yetu ya wimbo wa katikati leo inatuambia kwamba nafsi
yangu inakuonea kiu ee Bwana. Hii kweli ni sala ya mwenye imani; aliyekwisha
kuuonja wema wa Bwana na hivyo hataki kutengwa naye kabisa.
Huyu
mtu ni Paulo anavyojieleza katika somo la kwanza. Yeye basi anatoa ushuhuda
leo, kaishi hapa duniani katika ulinzi mkali kabisa wa Mwenyezi Mungu. Imefikia
mahali kuona kwamba hakuna tofauti ya kufa na kuishi. Yote ni mamoja-hii
ilikuwa ni dhihirisho kubwa la ukuu wa imani yake. Sisi tuombe kuwa kama Paulo
ndugu zangu. Ifikie mahali tuone kwamba maisha ni Kristo, kuishi au kufa yote
ni ya Mungu. Wengi hatujafikia hii hali. Hadi ile siku ya kufa tunakuwa na
hofu, tunaogopa, tunateseka, ni dhahiri kwamba bado hatujajikabidhi mikononi
mwa Mwenyezi Mungu na ndio tunaogopa. Hata baadhi ya wazee wa miaka tisini
wataogopa na mwishowe tunakuwa katika hofu.
Tuombe
Mungu leo tuachane na hofu hii, tujikabidhi mikononi mwake Mungu. Mungu atosha
kabisa.
Kwenye
injili Yesu anapinga watu kukaa kwenye viti vya mbele, kujitangazia utukufu
wenyewe kabla ya watu kuwatangazia huu utukufu, kujiita watakatifu kabla ya
kutangazwa. Yesu kwa hapa anakataza tabia ya kungangania mambo; kungangani ni
dhihirisho la hofu ndani ya roho ya mtu, dhihirisho la kukosekana kwa imani,
kutokujiamini kwamba nafasi yako itabakia na hivyo unaanza kuwahi mapema.
Lakini
anayejiamini hataanza kwa kuwahi kwani anajua kwamba nafasi yake ipo tu. Na
huyu anayeanza kwa kukaa kwenye nafasi ya mbele huishia kukosa kila kitu kwani
atakapokuwa ananyanyuka kurudi, atakuta hata ile nafasi ya nyuma
imekwishachukuliwa na wengine na ataishia kusimama. Ndivyo inavyotokea na kwetu
sisi pale tunapoanza kujiita watakatifu-tunaishia kukosa kila kitu kwani wakati
tunapohukumiwa na kuambiwa kwamba hatufai, unakuta hata ile nafasi ya kutubu haipo
tena kwani muda unakuta umekwisha na tunaishia kutupwa motoni.
Ukingangania
nafasi ya mbele unaishia kujisahau na kutoitambua hali yako na huishia kuanguka
zaidi. Leo tuangalie jinsi nafasi ya mbele inavyoangusha, jinsi ilivyotufanya
tuwadharau wenzetu, tuwanyanyase wenzetu na kusahau kutubu.
------------------------
Copyright
©2013-2020 ©FurKat, FurahayaKikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment