MASOMO
YA MISA, OKTOBA 18, 2022
IJUMAA, JUMA LA 28 LA MWAKA
SIKUKUU
YA MT. LUKA, MWINJILI
SOMO
1
2Tim.
4:10 – 17
Dema
aliniacha, akiupenda ulimwengu huu wa sasa, akasafiri kwenda Thesalonike;
Kreske amekwenda Galatia; Tito amekwenda Dalmatia. Luka peke yake yupo hapa
pamoja nami. Umtwae Marko, umlete pamoja nawe, maana anifaa kwa utumishi. Lakini
Tikiko nalimpeleka Efeso. Lile joho nililoliacha kwa Karpo huko Troa, ujapo
ulilete, na vile vitabu, hasa vile vya ngozi. Iskanda, mfua shaba, alionyesha
ubaya mwingi kwangu; Bwana atamlipa sawasawa na matendo yake. Nawe ujihadhari
na huyo, kwa sababu aliyapinga sana maneno yetu.
Katika
jawabu langu la kwanza hakuna mtu aliyesimama upande wangu, bali wote
waliniacha; naomba wasihesabiwe hatia kwa jambo hilo. Lakini Bwana alisimama
pamoja nami akanitia nguvu, ili kwa kazi yangu ule ujumbe utangazwe kwa utimilifu,
hata wasikie Mataifa yote.
Neno
la Bwana… Tumshukuru Mungu.
________
WIMBO
WA KATIKATI
Zab.
145:10 – 13, 17 – 18 (K) 12
(K)
Wacha wako, Ee Bwana, wajulisha matendo yako makuu na utukufu wa fahari ya
ufalme wako.
Ee
Bwana, kazi zako zote zitakushukuru,
Na
wacha Mungu wako watakuhimidi,
Wataunena
utukufu wa ufalme wako,
Na
kuuhadithia uweza wako. (K)
Ili
kuwajulisha watu matendo yake makuu,
Na
utukufu wa fahari ya ufalme wake.
Ufalme
wako ni ufalme wa zamani zote,
Na
mamlaka yako ni ya vizazi vyaote. (K)
Bwana
ni mwenye haki katika njia zake zote,
Na
mwenye fadhili juu ya kazi zake zote.
Bwana
yu karibu na wote wamwitao,
Wote
wamwitao kwa uaminifu. (K)
________
SHANGILIO
Yn.
15:1 – 9
Aleluya,
aleluya,
Ni
mimi niliyewachagua ninyi, nikawaweka mwende mkazae matunda, matunda yenu
yapate kukaa.
Aleluya.
________
INJILI
Lk.
10:1 – 9
Bwana
aliweka wengine, sabini, akawatuma wawili wawili wamtangulie kwenda kila mji na
kila mahali alipokusudia kwenda mwenyewe. Akawaambia, Mavuno ni mengi, lakini
watenda kazi ni wachache; basi mwombeni Bwana wa mavuno apeleke watenda kazi
katika mavuno yake. Enendeni; angalieni, nawatuma kama wanakondoo kati ya mbwa
mwitu. Msichukue mfuko, wala mkoba, wala viatu; wala msimwamkie mtu njiani. Na
nyumba yoyote mtakayoingia, semeni kwanza, Amani iwemo nyumbani humu; na
akiwamo mwana wa amani, amani yenu itamkalia; la, hayumo, amani yenu itarudi
kwenu. Basi, kaeni katika nyumba iyo hiyo, mkila na kunywa vya kwao; maana,
mtenda kazi amestahili kupewa ujira wake. Msihamehame kutoka nyumba hii kwenda
nyumba hii. Na mji wowote mtakaouingia, wakiwakaribisha, vileni vyakula
viwekwavyo mbele yenu; wapozeni wagonjwa waliomo, waambieni Ufalme wa Mungu
umewakaribia.
Neno
la Bwana… Sifa kwako Ee Kristo.
Copyright
© 2022, "MASOMO YA MISA" published by T.M.P. Book Department, Tabora
– Tanzania. Readings reproduced by Furaha ya Kikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com
No comments:
Post a Comment