“ASALI
ITOKAYO MWAMBANI”
Jumanne,
Oktoba 18, 2022
Juma
la 29 la Mwaka wa Kanisa
Sikukuu
ya Mt. Luka Mwinjili,
2
Tim 4:10-17
Zab
144:10-13, 17-18
Lk
10: 1-9
TUMEITWA
KUWA MASHAHIDI WA YESU!
Katika
Injili, Luka leo anatuonesha tena wengine sabini ambao Yesu anawatuma baada ya
kupokea maelekezo. Luka lazima atakuwa pia ni mmoja wapo wa Wafuasi waliotumwa
kwa utume. Ni vigumu kwa mtu ambaye hakuwa karibu na Yesu kufahamu namna hiyo
na kuweka katika mpangilio katika kumwelezea kama mtu mkamilifu.
Sisi
pia maagizo haya yanatolewa kwetu. Tunapaswa kujitoa kwa ufahamu wetu wote
kuhubiri Ufalme wa Mungu na sio kuyumbishwa na vitu vingine vidogo. Kufanya
haya ni lazima kusafiri na mwanga-chukua tu, vile vya muhimu na tuacha nyuma
yote ambayo yanaweza kutuharibu. Tunakaribishwa kufanya kazi hii, si kwasababu
ya chochote tutakachopata kutokana nayo, bali kwa yale tutakayo wapa wengine
bila malipo, bila kutegemea heshima Fulani au malipo flani. Bwana anataka
wafuasi wake wamtegemee yeye na sio kujitegemea wenyewe.
Sala:
Bwana, naomba furaha na ukweli wa Injili ubadili maisha yangu ili niweze kuutoa
ushuhuda kwa wale wote walioo karibu name. Amina
Copyright
©2013-2022 ©FurKat, Furaha ya Kikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com
No comments:
Post a Comment