MASOMO
YA MISA,
JUMATANO,
SEPTEMBA 10, 2025
JUMA
LA 23 LA MWAKA
________
SOMO
1
Kol.
3:1-11
Mkiwa
mmefufunuliwa pamoja na Kristo yatafuteni yaliyo juu, Kristo aliko, ameketi
mkono wa kuume wa Mungu. Yafikirini yaliyo juu, siyo yaliyo katika nchi. Kwa
maana mlikufa, na uhai wenu umefichwa pamoja na Kristo katika Mungu. Kristo
atakapofunuliwa, aliye uhai wetu, ndipo na ninyi mtafunuliwa pamoja naye katika
utukufu.
Basi,
vifisheni viungo vyenu vilivyo katika nchi, uasherati, uchafu, tamaa mbaya,
mawazo mabaya, na kutamani, ndiyo ibada ya sanamu; kwa ajili ya mambo hayo huja
ghadhabu ya Mungu. Katika hayo ninyi nanyi mlitembea zamani, mlipoishi katika
hayo. Lakini sasa yawekeni mbali nanyi haya haya yote, hasira, na ghadhabu, na
uovu, na matukano, na matusi vinywani mwenu. Msiambiane uongo, kw akuwa mmevua
kabisa utu wa kale, pamoja na matendo yake; mkivaa utu mpya, unaofanywa upya
upate upafamu sawasawa na mfano wake yeye aliuumba. Hapo hapana Myunani wala
Myahudi, kutahiriwa wala kutokutahiriwa, mgeni wala mshenzi mtumwa wala
mwungwana, bali kristo ni yote, na katika yote.
Neno
la Bwana… Tumshukuru Mungu.
________
WIMBO
WA KATIKATI
Zab.
145:2-3, 10-13 (K) 9
(K)
Bwana ni mwema kwa watu wote.
Kila
siku nitakuhimidi,
Nitalisifu
jina lako milele na milele.
Bwana
ndiye mkuu mwenye kusifiwa sana,
Wala
ukuu wake hautambulikani. (K)
Ee
Bwana, kazi zako zote zitakushukuru,
Na
wacha Mungu wako watakuhimidi.
Wataunena
utukufu wa ufalme wako,
Na
kuuhadithia uweza wako. (K)
Ili
kuwajulisha watu matendo yake makuu,
Na
utukufu wa fahari ya ufalme wake.
Ufalme
wako ni ufalme wa zamani zote,
Na
mamlaka yako ni ya vizazi vyote. (K)
________
SHANGILIO
Zab.
119:28,33
Aleluya,
aleluya,
Unitie
nguvu sawasawa na neno lako, Ee Bwana, unifundishe njia ya amri zako.
Aleluya.
________
INJILI
Lk.
6:20 – 26
Yesu
aliinua macho yake akawatazama wanafunzi wake, akasema,
Heri
ninyi mlio maskini, kwa sababu ufalme wa Mungu ni wenu.
Heri
ninyi mlio na njaa sasa, kwa sababu mtashiba.
Heri
ninyi mliao sasa, kwa sababu mtacheka.
Heri
ninyi watu watakapowachukia na kuwatenga, na kuwashutumu, na kulitupa nje jina
lenu kama neno ovu, kwa ajili ya Mwana wa Adamu.
Furahiwani
siku ile na kuruka-ruka, kwa kuwa, tazama, thawabu yenu ni kubwa mbinguni;
maana, baba zao waliwatenda manabii vivyo hivyo.
Lakini,
ole wenu ninyi mlio na mali, kwa kuwa faraja yenu mmekwisha kuipata.
Ole
wenu ninyi ambao mmeshiba sasa, kwa kuwa mtaona njaa.
Ole
wenu ninyi mnaocheka sasa, kwa kuwa mtaomboleza na kulia.
Ole
wenu ninyi watu wote watakapowasifu, kwa kuwa baba zao waliwatenda manabii wa
uongo mambo kama hayo.
Neno la Bwana… Sifa kwako Ee Kristo.
Copyright
© 2025, "MASOMO YA MISA" published by T.M.P. Book Department, Tabora
– Tanzania. Readings reproduced by Furaha ya Kikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com
No comments:
Post a Comment