“ASALI ITOKAYO MWAMBANI”
Afakari ya kila siku
Jumatano, Septemba 10, 2025
Juma la 23 la Mwaka wa Kanisa
Kumbukumbu ya Mt. Yohane Chrysostom, Askofu na Mwalimu wa Kanisa
Kol 3: 1-11;
Za 144: 2,3,10-13;
Lk 6: 20-26
BARAKA ZA HERI!
Kila moyo wa mwanadamu umeumbwa kwa ajili ya furaha. Mungu mwenyewe, katika
Utatu Mtakatifu, ndiye Furaha Kuu, ndiye Furaha yote. Masomo yetu ya leo
yanatuambia kwamba maskini wapo katika hali salama zaidi kuliko matajiri. Moyo
wa Mwanadamu, na uzuri wake na uwezo wake wakupata utakatifu, unachafuliwa,
unazimwa na kuharibiwa kwa kuwa mtumwa wa mali na anasa. Tamaa isiyo na
mpangilio ya fedha, nyumba, ardhi na vitu vimechafua furaha ya watu wengi na
pia furaha ya familia mbali mbali.
Leo Injili inaongelea pia kitu kingine kinachochafua roho nyingi: tamaa ya
anasa na kusifiwa (kujenga jina). “Ole wenu ninyi watu wote watakapo wasifu,
kwakuwa baba zao waliwatenda manabii wa uongo mambo kama hayo” (Lk 6: 26).
“heri yenu ninyi watu watakapo wachukia, na kuwatenga, na kuwashutumu, na
kulitupa nje jina lenu kama neno ovu, kwa ajili ya Mwana wa Adamu. Furahini na
kuruka-ruka, kwakuwa, tazama, thawabu yenu ni kubwa mbinguni, maana, baba zao
waliwatenda manabii [WA KWELI] vivyo hivyo.” (Lk 6: 22-23).
Yesu anataka kutuambia kwamba watu wakweli wanaomfuata watapata mateso
mengi, haitakuwa rahisi njia ya Yesu, mtu anapaswa kusema ukweli hata pale
inapo hatarisha maisha yake, kama vile manabii wa ukweli walivyoteseka zamani.
Sifa za nabii wa ukweli ni kwamba hakuambii kile ambacho unachotaka kusikia
bali anasema ukweli kwasababu ni ukweli. Manabii wengi walipoteza maisha yao
kwasababu waliitwa na wafalme ili kutoa unabii juu ya jambo Fulani, lakini wao
kwa ujasiri walisema ukweli hata kumrekebisha mfalme na hapo maisha yao yakawa
hatarini. Mfalme alitegemea kusikia akisifiwa tu, lakini manabii wa kweli
walisema ukweli, huu ndio wito anaotuambia Yesu. Tusiwe kama manabii wa uongo
wanaopenda kuongea tu kile ambacho watu wanapenda kusikia bali tuseme ukweli
kwasababu ni jambo la kweli.
Sala: Bwana, nisaidie mimi niweze kutafuta Baraka kutoka katika changanmoto
na magumu katika maisha. Badala ya kuona misalaba yangu kama uovu, nisaidie
mimi niweze kuona mkono wako ukifanya kazi katika kuyabadilisha na hivyo kupata
neema nyingi katika vitu vyote. Yesu, nakuamini wewe. Amina
No comments:
Post a Comment