MASOMO
YA MISA,
JUMATANO,
AGOSTI 20, 2025
JUMA
LA 20 LA MWAKA
Kumbukumbu
ya Mtakatifu Bernardo
________
SOMO
I
Amu
9: 6-15
Watu
wote wa Shekemu walikusanyika pamoja, na jamaa yote ya Milo, wakaenda na
kumtawaza Abimeleki awe mfalme, karibu na huo mgandi ulio karibu na ngome iliyo
katika Shekemu.
Kisha
walipomwambia huyo Yothamu, yeye akaenda, akasimama juu ya kilele cha kilima
cha Gerizimu, akapaza sauti yake, akapiga kelele, na kuwaambia:
Nisikieni
mimi, enyi watu wa Shekemu, ili kwamba Mungu naye apate kuwasikia ninyi.
Siku
moja miti ilitoka ili kuutia mmoja mafuta uwe mfalme juu yao; ikauambia mti
mzeituni, Tawala wewe juu yetu.
Lakini
huo mzeituni ukaiambia, Je! Niache mafuta yangu, ambayo kwangu mimi watu
wamheshimu Mungu na wanadamu, ili niende nikayongeyonge juu ya miti?
Kisha
miti ikauambia mtini, Njoo wewe, utawale juu yetu.
Lakini
huo mtini ukaiambia, Je! Niuache utamu wangu, na matunda yangu mazuri, niende
nitayonge-yonge juu ya miti?
Kisha
miti ikauambia mzabibu, Njoo wewe, utawale juu yetu.
Huo
mzabibu nao ukaiambia, Je! Niiache divai yangu, ambayo humfurahisha Mungu na
wanadamu, ili niende nikayonge-yonge juu ya miti?
Ndipo
hiyo miti yote ikauambia mti wa miiba, Njoo wewe, utawale juu yetu.
Huo
mti wa miiba ukaiambia miti, Kwamba ninyi mwanitia mafuta niwe mfalme juu yenu
kwelikweli, basi njoni mtumaini kivuli changu; na kwamba sivyo, na utoke moto
katika mti wa miiba na kuitekete mierezi ya Lebanoni.
Neno
la Bwana...Tumshukuru Mungu
________
WIMBO
WA KATIKATI
Zab.
21: 1-6
(K)
Ee Bwana, mfalme atazifurahia nguvu zako.
Ee
Bwana, mfalme atazifurahia nguvu zako,
Na
wokovu wako ataufanyia shangwe nyingi sana.
Umempa
haja ya moyo wake,
Wala
hukumzuilia matakwa ya midomo yake. (K)
Maana
umesogezea Baraka za heri,
Umemvika
taji ya dhahabu safi kichwani pake.
Alikuomba
uhai, ukampa.
Muda
mrefu wa siku nyingi, milele na milele. (K)
Utukufu
umemsogezea Baraka za heri,
Umemvika
taji ya dhahabu safi kichwani pake.
Alikuomba
uhai, ukampa.
Muda
mrefu wa siku nyingi, milele na milele. (K)
________
SHANGILIO
Zab
119:18
Aleluya,
aleluya,
Unifumbue
macho yangu niyatazame
maajabu
yatokayo katika sheria yako.
Aleluya.
________
INJILI
Mt.
20: 1-16
Yesu
aliwaambia wafuasi wake: Ufalme wa mbinguni umefanana na mtu mwenye nyumba,
aliyetoka alfajiri kwenda kuajiri wakulima awapeleke katika shamba lake la
mizabibu. Naye alipokwisha kupatana na wakulima kuwapa kutwa dinari,
aliwapeleka katika shamba lake la mizabibu. Akatoka mnamo saa tatu, akaona
wengine wamesimama sokoni wasiokuwa na kazi; na hao nao akawaambia, Enendeni
nanyi katika shamba langu la mizabibu, na iliyo haki nitawapa. Wakaenda.
Akatoka
tena mnamo saa sita na saa kenda, akafanya vile vile. Hata kama saa kumi na
moja akatoka, akauta wengine wamesimama, akawaambia, Mbona mmesimama hapa
mchana kutwa bila kazi? Wakamwambia, Kwa sababu hakuna mtu aliyetuajiri.
Akawaambia enendeni nanyi katika shamba la mizabibu.
Kulipokuchwa,
yule bwana wa shamba akamwambia masimamizi wake, Waite wakulima, uwalipe ujira
wao, ukianzia wa mwisho hata wa kwanza. Na walipokuja wale wa saa kumi na moja,
walipokea kila mtu dinari. Na wale wa kwanza walipokuja, walidhani kwamba
watapokea zaidi; na hao pia wakapokea kila mtu dinari.
Basi
wakiisha kuipokea, wakamnung’unukia mwenye nyuma, wakisema, Hao wa mwisho
wametenda kazi saa moja tu, nawe umewasawazisha na sisi tuliostahimili taabu na
hari za mchana kutwa. Naye akamjibu mmoja wao, akamwambia, Rafiki, sikudhulumu;
hukupatana nami kwa dinari? Chukua iliyo yako, uende zako; napenda kumpa huyu
wa mwisho sawa na wewe. Si halali yangu kutumia vilivyo vyangu kama nipendavyo?
Au jicho lako limekuwa ovu kwa sababu ya mimi kuwa mwema Vivyo hivyo wa mwisho
watakuwa wa kwanza, na wa kwanza watakuwa wa mwisho.
Neno
la Bwana...Sifa kwako, ee Kristo
Copyright
© 2025, "MASOMO YA MISA" published by T.M.P. Book Department, Tabora
– Tanzania. Readings reproduced by Furaha ya Kikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com
No comments:
Post a Comment