“ASALI
ITOKAYO MWAMBANI”
Tafakari
ya kila siku
Jumatano,
Agosti 20, 2025
Juma
la 20 la Mwaka
___________________
Amu
9: 6-15;
Zab
20: 2-7;
Mt
20:1-16
___________________
JE,
UNAKUWA NA WIVU MWENZAKO ANAPO FANIKIWA?
Somo
la Injili ni maelezo ya mfano wa wakulima katika shamba la mizabibu. Mfano
unaeleza ni kwa jinsi ghani mwenye shamba alivyoenda sokoni kwa muda tofauti
tofauti na kutafuta wafanyakazi hata wakati wa saa kumi na moja jioni. Wakati
wale wafanyakazi wa kwanza walikuwa wamekubaliana kabisa kwamba watapewa
mshahara wa dinari moja, na wakati wengine wakiambiwa watapewa kilicho haki
yao. Wakati wa malipo macho yalikuwa kwa wale ambao wameajiriwa wa mwisho,
wakati wale wa kwanza wakilipwa mbele ya wengine wote. Wa mwisho wanalipwa sawa
kama walivyokubaliana na mwenye shamba. Ingawaje mfano hausemi ni kiasi gfhani
cha kazi kilicho fanyika au pengine wale wa mwisho walifanya kazi haraka haraka
kiasi cha kuwafikia wale wa kwanza? Hausemi. Hali hii inaleta changamoto!
Lakini Yesu alitaka kusema kwamba wadhambi na watoza ushuru walio tubu watakuwa
pia katika hali moja na wale ambao wameshika sheria tangu mwanzoni. Mfano huu
unataka kutufundisha kitu kwamba, Mungu haangalii ni kwa muda ghani uliofanya
kazi, bali ni kwa jinsi ghani ulivyo mwaminifu katika kazi.
Kwanza
kabisa, hali hii inashawishi kila mtu kuwa na wivu. Wivu ni aina ya kuwa na
huzuni au kutokufurahi kwasababu ya mtu mwingine kufanikiwa. Pengine tunaweza
kuelewa wivu waliokuwa nao wale waliofanya kazi siku nzima. Ukweli si kwamba ni
kitu ghani walichopokea bali ni wale wengine wamepokea kiasi hicho hicho kama
wao, hivyo inaonekana kuwa kama sio haki. Tofatuti ni kwamba wale wa kwanza
wamepokea kile walicho kifanyia kazi siku nzima, na wengine wamepokea sawa na
hao wengine kwasababu ya ukaribu wa Bwana shamba.
Kama
sisi tutajiweka na lile kundi linalo lalamika, ni vizuri tuangalie misukumo
yetu. Je, sisi tunaweza kujazwa furaha na Amani kwasababu ya ndugu zetu kufanikiwa?
Je, waweza kumshukuru Mungu na kumwambia asante wakati ndugu au mwingine alivyo
fanikiwa? Wivu mbaya ni dhambi, na ni dhambi ambayo inatuacha tukiwa hatuja
ridhika na wenye huzuni. Njia pekee ambayo tunaweza kushinda ni kufurahia
mafanikio ya ndugu zetu.
Sala:
Bwana, ninatenda dhambi na ninakubali kwamba nina wivu moyoni mwangu.
Ninakushukuru wewe kwa kunisaidia kuliona hili ninakuomba unisaidie sasa
nikabidhi kwako. Tafadhali nisaidie kuondoa kwa kuwa na shukrani kwa neema na
huruma yako unawajalia wengine. Yesu, nakuamini wewe. Amina
No comments:
Post a Comment