MASOMO
YA MISA, AGOSTI 2, 2025
JUMAMOSI,
JUMA LA 17 LA MWAKA
SOMO
1
Wal.
25:1,8-17
Bwana
alinena na Musa katika mlima wa Sinai, na kumwambia: Utajihesabia sabato za
miaka, maana, miaka saba mara saba; zitakuwa ni siku za sabato saba za miaka
kwenu, maana miaka arobaini na kenda. Ndipo utakapoipeleka pande zote hiyo
baragumu yenye sauti kuu, siku ya kumi ya mwezi wa saba; katika siku hiyo ya
upatanisho mtaipeleka baragumu katika nchi yenu yote. Na mwaka wa hamsini
mtautakasa, na kupiga mbiu ya kuachwa mahuru katika nchi yote kwa watu wote
waiketio; itakuwa ni yubile kwenu; nanyi kila mtu atairudia milki yake
mwenyewe, nanyi mtarejea kila mtu kwa jamaa yake. Mwaka huo wa hamsini utakuwa
ni yubile kwenu; msipande mbegu, wala msivune kitu hicho kimeacho chenyewe,
wala msizitunde zabihu za mizabibu isiyopelewa. Kwa kuwa ni yubile; utakuwa
mwaka mtakatifu kwenu; mtakula maongeo yake yatokayo shambani.
Mwaka
huo wa yubile mtairudia kila mtu milki yake. Tena kama ukimwuzia jirani yako
chochote, au kununua chochote mkononi mwa jirani yako, msidanganyane wenyewe
kwa wenyewe; kwa hesabu ya miaka iliyo baada ya yubile ndivyo utakavyonunua kwa
jirani yako, na kama hesabu ya miaka ya mavuno ndivyo atakavyokuuzia wewe. Kama
hesabu ya miaka ilivyo ni nyingi ndivyo utakavyoongeza bei yake, na kama hesabu
ya miaka ilivyo ni chache ndivyo utakavyopunguza bei yake; kwani yeye akuuzia
mavuno kama hesabu yake ilivyo. Wala msidanganyane; lakini utamcha Mungu wako;
kwa kuwa mimi ndimi Bwana, Mungu wenu.
Neno
la Bwana... Tumshukuru Mungu.
WIMBO
WA KATIKATI
Zab.
67:1-2, 4- 6-7 (K) 3
(K)
Watu na wakushukuru, Ee Mungu, Watu wote na wakushukuru.
Mungu
na atufadhili na kutubariki,
Na
kutuangazia uso wake.
Njia
yake ijulikane duniani,
Wokovu
wake katikati ya mataifa yote. (K)
Mataifa
na washangilie,
Naam,
waimbe kwa furaha,
Maana
kwa haki utawahukumu watu,
Na
kuwaongoza mataifa walioko duniani. (K)
Nchi
imetoa mazao yake;
Mungu,
Mungu wetu, ametubariki.
Mungu
atatubariki sisi;
Miisho
yote ya dunia itamcha Yeye. (K)
SHANGILIO
Zab.
25:4,5
Aleluya,
aleluya,
Ee
Bwana, unijulishe njia zako, unifundishe mapito yako.
Aleluya.
INJILI
Mt.
14:1 – 12
Mfalme
Herode alisikia habari za Yesu, akawaambia watumishi wake, Huyo ndiye Yohane
Mbatizaji; amefufuka katika wafu; na kwa hiyo nguvu hizo zinatenda kazi ndani
yake.
Maana
Herode alikuwa amemkamata Yohane, akamfunga, akamtia gerezani, kwa ajili ya
Herodia, mke wa Filipo nduguye. Kwa sababu Yohane alimwambia, Si halali kwako
kuwa naye. Naye alipotaka kumwua, aliwaogopa watu, maana walimwona Yohane kuwa
nabii. Hata ilipofika sikukuu ya kuzaliwa kwake Herode, binti Herodia alicheza
mbele ya watu, akampendeza Heorode. Hata akaahidi kwa kiapo ya kwamba atampa
lolote atakaloliomba. Naye, huku akichochewa na mamaye, akasema, nipe hapa
katika kombe kichwa cha Yohane Mbatizaji.
Naye
mfalme akasikitika; lakini kwa ajili ya viapo vyake, na kwa ajili ya wale
walioketi chakulani pamoja naye, akaamuru apewe; akatuma mtu akamkata kichwa
Yohane mle gerezani. Kichwa chake kikaletwa katika kombe, akapewa yule kijana;
akakichukua kwa mamaye. Wanafunzi wake wakaenda, wakamchukua yule maiti,
wakamzika; kisha wakaenda wakampasha Yesu habari.
Neno
la Bwana... Sifa kwako Ee Kristo.
Copyright
© 2025, "MASOMO YA MISA" published by T.M.P. Book Department, Tabora
– Tanzania. Readings reproduced by Furaha ya Kikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com
🙏🏽
ReplyDelete