ASALI
ITOKAYO MWAMBANI”
Tafakari
ya kila siku
Jumamosi,
Agosti 2, 2025
Juma
la 17 la Mwaka wa Kanisa
Wal.
25:1,8-17
Zab
67:2-3,5-8
Mt.
14:1-12
CHUKI
NA KISASI
Katika
somo la Injili la leo tunasikia kuhusu kukatwa kichwa kwa Yohane Mbatizaji
kwasababu ya ombi la Salome, binti wa Herodia. Yohane alikuwa gerezani
kwasababu ya kuongea ukweli kuhusu Herodi kumchukua mke wa nduguye, na hivyo
Yohane alichukiwa na Herodia. Hivyo mtoto wa Herodia alivyo cheza vizuri mbele
ya Herodi Mfalme na wageni wake, Herodi alipendezwa sana na kucheza kwa binti
huyu na hivyo kumwambia aombe lolote kwake naye binti anaomba kichwa cha Yohane
mbatizaji baada ya kuomba ushauri kwa mama yake. Hivyo kwanini Herodia na mtoto
wake wanaomba kichwa cha Yohane Mbatizaji?
Herodi
alikuwa mtu wa kidunia. Pengine Herodia alikuwa na vinywaji vingi sana siku hiyo
katika siku hii yake ya kuzaliwa; na katika furaha hii anafanya uamuzi ambao
sio wa hekima, ambao Herodia anatumia muda huu kutimiza maovu yake. Herodi
anafanya uamuzi ambao yeye mwenyewe hakutaka hivyo anaogopa kutenda mema.
Anajazwa na chuki ya mke wake huyu na hivyo, anaamua Yohane akatwe kichwa yeye
ambaye alikuwa amemzoea kumsikiliza na kufurahi. Herodia hakuwa na dhamiri hai
yenye kumkataza kufanya uovu. Aina hii ya chuki inaeleza jinsi ghani chuki
ilivyo mbaya inavyokuwa kubwa huleta madhara. Wakati hasira inavyokuwa huleta
madhara makubwa mno na kusababisha uharabifu mkuwa sana katika maisha yetu na
ya watu. Hali hii ya hasira inapaswa kufanyiwa toba na kusamehewa mwanzoni
kabisa kabla haijawa kubwa.
Tafakari
leo, je, umeshikilia hasira ambayo ni mbaya na kinyongo moyoni mwako katika
hali yeyote? Je, hasira hiyo inakuwa nakusababisha hasara kwako na kwa wengine?
Kama ndiyo hivyo, jitahidi kuiacha na samehe na anza maisha mapya. Ndilo jambo
jema ambalo waweza kulifanya.
Sala:
Bwana, ni pe neema ninayo hitaji ili niweze kutazama moyo wangu au uchungu
wowote ndani yangu au chuki yeyote ile. Nisafishe Bwana na nakuomba unifanye
niwe huru. Yesu, nakuamini wewe. Amina
🙏🏽
ReplyDelete