Everyday Saint / Maisha ya Watakatifu

MASOMO YA MISA, JUNI 22, 2025



MASOMO YA MISA, JUNI 22, 2025
SHEREHE YA MWILI NA DAMU TAKATIFU YA BWANA WETU YESU KRISTO


SOMO 1
Mwanzo 14:18-20

Melkizedeki mfalme wa Salemu alileta mkate na divai, naye alikuwa kuhani wa Mungu Aliye juu sana. Akambariki, akasema, Abramu na abarikiwe na Mungu Aliye juu sana, Muumba mbingu na nchi. Ahimidiwe Mungu Aliye juu sana, aliyewatia adui zako mikononi mwako. Abramu akampa fungu la kumi la vitu vyote.

Neno la Bwana... Tumshukuru Mungu.


WIMBO WA KATIKATI
Zaburi 110:1-4 (K) 4

(K) Ndiwe kuhani hata milele, Kwa mfano wa Melkizedeki.

Neno la Bwana kwa Bwana wangu
Uketi mkono wangu wa kuume
Hata niwafanapo aui zako
Kuwa chin ya mikuu yako (K)

Bwana atainyosha toka Sayuni 
Fimbo ya nguvu zako, 
Uwe na enzi kati ya adui zako. (K)

Kwa uzuri wa utakatifu, 
Tokea tumbo la asubuhi, 
Unao umande wa ujana wako. (K)

Bwana ameapa, 
Wala hataghairi, 
Ndiwe kuhani hata milele, 
Kwa mfano wa Melkizedeki. (K)


SOMO 2
1 Wakorinto 11:23-26

Mimi nalipokea kwa Bwana niliyowapa nanyi, ya kuwa Bwana Yesu usiku ule aliotolewa alitwaa mkate, naye akiisha kushukuru akaumega, akasema, Huu ndio mwili wangu ulio kwa ajili yenu; fanyeni hivi kwa ukumbusho wangu. Na vivi hivi baada ya kula akakitwaa kikombe, akisema. Kikombe hiki ni agano jipya katika damu yangu; fanyeni hivi kila mnywapo, kwa ukumbusho wangu. Maana kila mwulapo mkate huu na kukinywea kikombe hiki, mwaitangaza mauti ya Bwana hata ajapo.

Neno la Bwana... Tumshukuru Mungu.


SHANGILIO
Yohana 6:51

Aleluya, Aleluya!
Mimi ndimi chakula chenye uzima kilichoshuka kutoka mbinguni;
asema Bwana; mtu akila chakula hiki, akaishi milele.
Aleluya!


INJILI
Luka 9:11-17

Makutano walimfuata Yesu; akawakaribisha, akawa akisema nao habari za ufalme wa Mungu, akawaponya wale wenye haja ya kuponywa. Na jua likaanza kushuka; wakamwendea wale Thenashara, wakamwambia, Uage mkutano, ili waende katika vijiji na mashamba ya kandokando wapate mahali pa kulala na vyakula, maana hapa tulipo ni nyika tupu. Akawaambia, Wapeni ninyi chakula. Wakaswema, Hatuna kitu zaidi ya mikate mitano na samaki wawili, tusipokwenda tukawanunulie watu hawa wote vyakula. Kwa kuwa wanaume waliokuwako walipata kama elfu tano. Akawaambia wanfunzi wake, Waketisheni watu kwa safu, kila safu watu hamsini. Wakafanya hivyo, wakawakettisha wote. Akaitwaa ile mikate mitano na wale samaki wawili, akatazama juu mbinguni akavibariki, akavimega, akawapa wanafunzi wake ili wawaandikie mkutano. Wakala, wakashiba wote; na katika vile vipande vilivyowabakia walikusanya vikapu kumi na viwili.

Neno la Bwana... Sifa kwako Ee Kristo.


Copyright © 2025, "MASOMO YA MISA" published by T.M.P. Book Department, Tabora – Tanzania. Readings reproduced by Furaha ya Kikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com

No comments:

Post a Comment