
“ASALI ITOKAYO MWAMBANI”
Jumatano, Mei, 14, 2025,
Juma la 4 la Pasaka
Sikukuu ya Mtakatifu Matia Mtume
Mdo 1: 15-17, 20-26;
Zab,113: 1-8 (k.8);
Yn 15: 9-17.
VYOMBO VYA UPENDO!
“Hakuna upendo uliyo mkuu kuliko huu, wa mtu kuutoa uhai wake
kwaajli ya rafiki zake”. Upendo wa Yesu ni wa pekee na unajifunua kwa majitoleo
yake pale msalabani. Upendo wa Yesu ni sadaka na hauna masharti. Yuda
hakuutambua upendo huo, lakini sisi tunaitwa kuutambua kama wafuasi wa Kristo.
Kuwa mfuasi wa Kristo kuna mambo matatu yanayo jitokeza katika
Injili ya leo, kwanza kabisa, kila Mkristu ana wito wa pekee wakupendana na
mwezake. Na pili kila Mkristu ana wajibu wakumfuata Kristo na kutembea katika
njia yake ya utakatifu na upendo. Na mwisho kabisa kila Mkristo anapaswa
kujiunga na Mungu daima kwa njia ya sala.
Tumuombe mtakatifu Matia mtume tunae muadhimisha leo atuombee kwa
Mungu tuweze kuyashika hayo kama yeye alivyofanikiwa kuyashika kama mtume wa
Kristo aliyechukuwa ile nafasi ya Yuda Iskariote.
Sala: Yesu, naomba unisaidie mimi niweze kuwa chombo cha upendo
kama mtakatifu Matia mtume. Amina.
No comments:
Post a Comment