“KUFUFUKA NA KRISTO”
Tafakari ya Pasaka
Ijumaa, Mei 12, 2023,
Juma la 5 la Pasaka
Mdo 15: 22-31;
Zab 57: 8-12 (K. 10);
Yn 15: 12-17.
TUMECHAGULIWA KUWA WA MUNGU!
Watoto wanapenda kucheza michezo. Wakati mchezo unaundwa
kwa pande mbili, watoto wanaunga mstari wakisubiri kuchaguliwa. Kila mtoto
anategemea kuchguliwa wa kwanza. Inaonesha hamu ya ndani ya kutaka kuchaguliwa
kwa ajili ya mchezo. Hili linaonesha hamu iliyopo ndani ya kila mmoja wetu ya
kuchaguliwa. Uzuri ni kwamba, Mungu anamchagua kila mmoja wetu. Anatutaka sisi
kuwa watoto wa familia yake na anatutaka tuwe watu wake. Hili ni la muhimu
kulielewa na likieleweka linadhihirika. Mungu alituchgua sisi hata kabla hatuja
zaliwa. Anatufahamu kabla, tangu milele yote na anaweka jicho lake juu yetu,
akilenga kutuleta sisi katika kundi lake. Tunapaswa kutambua hili, kulikubali
na kuliamini. Sisi ni wake.
Mungu hatuchagui sisi tu kuwa wake, anatuchagua pia kwa
utume. Anataka kututumia sisi tuzae matunda kwa Ufalme wake. Anataka kututumia
sisi kwa malengo matakatifu na wito wa Kimungu. Haijalishi ni mara ngapi
tunaweza kujiona “hatustahili” tunaweza kujisikia kufanya utofauti, tunapaswa
kukumbuka kuwa Mungu hatuoni katika hali hiyo. Bali, anaona utajiri mkubwa
ndani ya kila mmoja wetu na kuchagua kutumia utajiri huo kujenga ufalme
wake.
Mungu anakuambia “nimekuchagua wewe” na “Nenda ukazae
matunda”. Kukubali wito wako kutoka kwa Mungu utabadilisha maisha yako na pia
yatabadilisha maisha ya wale ulioitwa kuwatumikia.
Sala: Bwana, ninatambua umenichagua mimi. Ninakubali wito
wako katika maisha yangu. Ninakubali ukweli kwamba umenichagua mimi katika hali
ya utume wa pekee na hali ya utukufu wa pekee. Nisaidie daima niendelee kusema
“ndio” kwa wito wako. Yesu, nakuamini wewe. Amina.
Copyright ©2013-2023 ©FurKat, Furaha ya
Kikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com
No comments:
Post a Comment