“KUFUFUKA NA KRISTO”
Tafakari ya Pasaka
Jumatatu, Mei 20, 2019.
Juma la 5 la Pasaka
Mdo 14:5-18;
Zab 115:1-4,15-16 (K. 1);
Yn 14:21-26.
MUNGU ANAISHI NDANI MWETU!
Watoto huwa wanaelewa kwamba Mungu anaishi ndani ya mioyo
yao. lakini, kama ukiwauliza wamejuaje, utaona wanakutazama kama
kuchanganyikiwa katika kujibu. Licha ya hayo, wao wanatambua kwamba Mungu anaishi
ndani yao. Pengine wewe utajibu nini katika swali hili kwamba, “umejuaje Mungu
anaishi ndani mwako?” Pengine unaweza kujikuta ukipotea katika kuelezea hali
hii ya juu ya fumbo la Imani yetu. Tunatambua kwamba Mungu anapenda kushikilia
mioyo yetu, kuongea na sisi, kutuimarisha, kutuongoza na kutulinda sisi.
Tunatambua kwa zawadi ya Imani yetu, kwamba Mungu yupo na anatamani muunganiko
wa ndani na sisi. Tunatamua tu hilo.
Imani inatuongoza kwenye uelewa, na kila mara tunapo
isikiliza sauti ya Mungu inayo ongea ndani mwetu, ikituongoza na kutulinda
sisi, ni mwanzo wa kuanza kuelewa kuishi kwake ndani mwetu. Kama Mt. Agustino
anavyosema, “Imani ni kuamini kile usicho kiona. Na matokeo ya imani ni kuona
kile unacho kiamini”. Imani kwa uwepo wa Mungu inatuongoza kwenye jibu la swali
hapo juu. Nitafahamuje, Mungu anaishi ndani mwangu? Jibu ni kwamba ni kwasababu
namuona ndani yangu, naongea na yeye ndani, na anaongea na mimi ndani. Na pia
naona matokeo ya Imani yangu kwake kutokana na kuamini huku.
Muache yeye aongee na wewe, katika maongezi ya ndani,
ruhusu kuishi kwake ndani kukuwe na kuthihirika kwa wengine. Mungu hapendi tu
kuthihirika ndani mwako lakini pia anataka kungara kupitia wewe.
Sala: Bwana, njoo uishi moyoni mwangu. Fanya moyo wangu
sehemu yako ya kuishi. Nisaidie niweze kukuona wewe hapo na kuongea na wewe na
kukupenda wewe ndani ya roho yangu. Yesu nakuamini wewe. Amina.
Copyright ©2013-2023 ©FurKat, Furaha ya
Kikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com
No comments:
Post a Comment