
“MBEGU ZA UZIMA”
Jumapili, Mei 11, 2025.
Dominika ya 4 ya Pasaka
Mdo 13: 14, 43-52;
Zab 100: 1-3, 5;
Ufu 7: 9, 14-17;
Yn 10: 27-30.
MCHUNGAJI MWEMA ANAITA
KONDOO WAKE!
Dominika ya nne ya
kipindi cha Pasaka, inajulikana kama “Dominika ya Kristo Mchungaji mwema”,
Injili inachukuliwa kutoka sura ya 10 ya Yohane ambapo Yesu anazungumza juu ya
yeye mwenyewe kama "Mchungaji Mwema". Yesu ametupa takwimu ya
Mchungaji Mwema ambaye anajua kondoo wake anawaita, yeye huwalisha na
anawaongoza wao. Kwa sababu hii, Kanisa linachukulia Dominika hii kuwa maalumu
kuwa “Siku ya Kuombea Miito Duniani”.
Leo, Kanisa zima
linatukumbusha hitaji letu kuomba, kama Yesu mwenyewe alivyo waambia wanafunzi
wake, hivyo kwamba "mwombeni Bwana wa mavuno apeleke watenda kazi katika
mavuno yake" (Lk 10: 2). Tangu hapo awali Kanisa “ kwa asili yake ni
umisionari" (Ad Gentes, 2), wito wa Ukristo unazaliwa ndani ya watu
kutokana na kazi ya umisionari. Kusikia na kufuata sauti ya Kristo Mchungaji
mwema, maana yake ni kuruhusi tuvutwe naye na tuongozwe naye, kujiweka wakfu
kwake maana yake kumruhusu Roho Mtakatifu kututumia sisi katika mabadiliko haya
ya umisionari, na kuamsha ndani yetu tamaa, furaha na ujasiri wa kutoa maisha
yetu wenyewe katika utumishi wa Ufalme wa Mungu.
Katika mzizi wa kila
wito wa Kikristo tunaona harakati hii ya msingi, ya kuacha nyuma faraja yetu na
mambo yote yanaotupendezesha nafsi zetu na kukita maisha yetu katika Yesu
Kristo. Ina maana ya kuondoka, kama Ibrahimu, na kuacha sehemu yetu ya asili na
kwenda mbele kwa uaminifu, tukijua kwamba Mungu atatuonesha njia ya nchi mpya.
Hii "kwenda mbele" isi tazamwe kama ishara ya mpango tu wa maisha ya
mtu binafsi, hisia ya mtu, utu wa mtu mwenyewe. Kinyume chake, wale ambao
wanamfuata Kristo wanapata uzima kwa wingi kwa kujiweka wenyewe bila kujibakiza
katika utumishi wa Mungu na ufalme wake. Wito wa Kikristo kwanza kabisa ni wito
wa upendo, upendo ambao hutuvuta sisi na kutuelekeza nje ya sisi wenyewe.
Kuitika wito wa Mungu, maana yake kumruhusu yeye atusaidie kujiacha wenyewe
kwakuondokana na usalama wetu wa uongo, na kutoka nje na kuenenda kwenye njia
inayo ongoza kwa Yesu Kristo, aliye asili na hatima ya maisha yetu na furaha
yetu.
Katika siku hizi kwanza
tunaombwa tuombee Kanisa liweze kupata wachungaji wema na waadilifu wa kufanya
kazi ya Kristo ya kueneza Injili, na kwamba Kanisa liweze kupata vijana wengi
wanoitwa kwenye wito wa upadre na utawa ikiwa ni pamoja na watoto wetu wenyewe.
Sala: Baba wa huruma,
uliyemtoa mwanao kwaajili ya wokovu wetu na ambaye anatutia nguvu kila wakati
kwa zawadi ya Roho wako, tujaliye sisi jumuiya ya Wakristo tulio hai, upendo na
furaha, vilivyo vya muhimu kwa maisha ya kindugu, na vinavyojenga ndani ya wadogo
mwamko wa wito wakujitoa wenyewe wakfu kwako na kwaajili ya wito wa uenezaji wa
neno lako.
No comments:
Post a Comment