Everyday Saint / Maisha ya Watakatifu

KUVUTWA KWA YESU!


“KUFUFUKA NA KRISTO”
Tafakari ya Pasaka
Alhamisi, Aprili 18, 2024
Juma la 3 la Mwaka

Mdo 8:26-40;
Zab 66:8-9,16-17,20 (K. 1);
Yn 6:44-51.


KUVUTWA KWA YESU!

Karl Rahner anasema, “kila ninapo ongea kuhusu mimi najikuta nikiongelea kuhusu Mungu, na kila ninapo ongelea kuhusu Mungu najikuta naongea kuhusu mimi”. Safari ya maisha yetu pia karibia ni kuvuta kila kitu na kila mtu kwangu. Katika ulimwengu huu ambao kila mtu yupo na shughuli zake ni rahisi sana kuruhusu sauti mbali mbali zituharibu. Ni rahisi kusikia kusukumwa huku na kule katika ulimwengu na mambo yake yote. Ulimwengu umekuwa mzuri sana ukiteka mipango yetu yote na kutupatia kuridhika kwa haraka lakini utatuacha bila kitu.

Lakini sauti ya Mungu na mwaliko wake ni tofauti. Unapatikana katika ukimya wa ndani. Lakini haina maana kwamba unapaswa kuwa katika monasteri ili kupata ukimya huu wa ndani. Unapatika katika uaminifu mkubwa katika sala kila siku, na tabia ya kurudi kwa Mungu kila wakati katika vitu vyote. Unapatikana tunapo jibu wito wa Mungu, na kuifuata, na kurudia tena kila mara. Hili linajenga tabia ya kuvutwa karibu, kusikia, na kuitika na kuvutwa karibu na kusikiliza na kuitika tena na tena.

Katika Injili ya leo, tunatambua kuwa tumeumbwa kwa sura na mfano wa Mungu, na tunavutwa daima kwa Mungu. Ndani kabisa mwa moyo wa Mwanadamu, ana mtamani Mungu. Ndio maana Yesu anasema wazi kwamba “hakuna ajaye kwangu asipovutwa na Baba yangu” (Yn 6: 44). Katika somo la kwanza tunamuona Ofisa wa Ethiopia wakati akisoma chuo cha nabii Isaya, anakutana na ukweli katika Maandiko Matakatifu kwa msaada wa Filipo, na baadae anamkubali Yesu kama Mkombozi na Bwana.

Tutenge muda tuvutwe kwa Yesu. Tenga muda mchache au zaidi kila siku wa ukimya. Funga macho na jisikilize. Msikilize Mungu akiongea na wewe. Wakati akikuvuta kwake itika kwa ukarimu. Huu ndio uchaguzi mzuri kabisa ambao waweza kufanya kila siku!

Sala: Bwana, naomba univute karibu ili niweze kutambua sauti yako. Ninapo kusikia ukiita, nisaidie niweze kukuitikia kwa ukarimu. Maisha yangu ni yako, Bwana mpendwa. Yesu, nakuamini wewe. Amina.


Copyright ©2013-2024 ©FurKat, Furaha ya Kikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com

No comments:

Post a Comment