“KUFUFUKA NA KRISTO”
Tafakari ya Pasaka
Alhamisi, Mei 11, 2023.
Juma la 5 Pasaka
Mdo 15: 7-21;
Zab 96: 1-3,10 (K. 3);
Yn 15: 9-11.
KUONGEA LUGHA YA MUNGU!
Wanadamu wanatamani kupendwaa na kujaliwa. Lakini ni
vigumu kwa njaa ya upendo kutimizwa, katika hali ya kibinadamu. Leo, Yesu
anaongea kuhusu upendo unaozalisha furaha isiyo pimika, ambayo ni Baba na Yeye
anayo tu kwa wale walio wake. Hatuwezi kumzidi Mungu kwa mapendo kwasababu
anatupenda bila kipimo, kwa upendo unaotoa neema, uzima, Amani na furaha.
Upendo wa Mungu ni kamili na hauwezi kuingiliwa. Upendo
wa Baba kwa Mwanae ni kamili katika nyanja zote. Hauna masharti na unakamilisha
yote. Ni kamili na hauna ubinafsi. Kwa kupokea upendo wa Baba, Yesu alipokea
yote aliyo hitaji. Upendo aliopokea Yesu kutoka kwa Baba yake hauwezi
kuondolewa. Hauwezi kuwekwa kwa ubinafsi. Unatiririka kutoka katika moyo wa
Yesu na kuja kwetu. Mtiririko huu wa upendo, tuliopewa sisi, hauwezi kufungwa
ndani ya mioyo yetu bila kwenda kwa wengine. Hivyo kama tunataka kuwa wapokeaji
wa zuri wa upendo wa Baba na Mwana, tunapaswa kuruhusu upendo huo uwatiririkie
wengine bila “Kikomo” na bila “Masharti”.
Leo tunaitwa kupenda kwa niaba ya upendo wenyewe, kwa
niaba ya Kristo, ambaye ndiye msingi wa upendo wa kweli. Si kwasababu nyingine
bali kwa upendo kamili ambao Yesu alitoa kwa ajili yetu. Maisha yetu kama
wafuasi wa Yesu yanapaswa kuwa maisha ya kujitoa kwa upendo kwa wengine. Upendo
wa Yesu ambao upo ndani yetu unapaswa kutambuliwa, kukukubali na kuupeleka kwa
wengine. Hili ndilo lengo la maisha ya Kikristo: kubaki katika upendo wa Kristo
na kujazwa furaha. Mimi na wewe tumebarikiwa kufahamu ukweli kwamba MUNGU ni
UPENDO. Hivyo tutangaze ukweli huu bila wasi wasi na bila kujibakiza. Kama
tutamruhusu Mungu atupende kwa upendo mkamilifu, tutaanza kuona mara moja
kwamba upendo huu ukitiririka ndani mwetu kama vile mto wa neema na huruma.
Sala: Bwana, ninakupenda wewe na ninatambua napendwa na
wewe. Nisaidie mimi niweze kuwa wazi kwa upendo wako. Nisaidie niweze kufanya
upendo huo uzame ndani ili uweze kutiririka kutoka moyoni mwangu na kwenda kwa
wengine pia. Yesu, nakuamini wewe. Amina
Copyright ©2013-2023 ©FurKat, Furaha ya
Kikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com
No comments:
Post a Comment