“KUFUFUKA NA KRISTO”
Tafakari ya Pasaka
Ijumaa, Aprili 19, 2024
Juma la 3 la Pasaka
Mdo 9:1-20;
Zab 117:1-2 (K. Mk 16:15);
Yn 6:52-59.
MAISHA YETU YANATOKA KWA KRISTO!
Mt. Paulo ambaye tunamsikia katika somo la
kwanza la leo alikuwa mtu mwenye Elimu ya juu/ busara aliyesoma chini ya
mwalimu mkuu Gamaliel. Uongofu wake wa ghafla ulitokea barabarani
akielekea Dameski. Paulo ambaye alikuwa na mambo mengi, lakini akikosa jambo
muhimu zaidi ambalo alilipata kupitia ndani ya tukio hili la wongofu. Alimpata
Yesu Kristo. Baada ya uzoefu huo Paulo anatangaza, "Kwangu mimi, kuishi ni
Kristo"; kama nilivyo, maisha ni Yesu Kristo" au "Naweza
kufanya yote katika Yeye anitiaye nguvu." "Naishi sasa si kwa
maisha yangu mwenyewe bali kwa maisha ya Kristo anayeishi ndani yangu."
Mara baada ya Paulo kukutana na Yesu, maisha
yake hayakubaki kamwe jinsi yalivyo kuwa mwanzo. Alibadilika kabisa. Alikuwa
kiumbe kipya katika Kristo. Nasi pia tunampokea Kristo katika Ekaristi
Takatifu. Ni kwa kiasi gani Ekaristi inabadilisha maisha yetu? Ni kwa kiasi
gani najitoa mwenyewe kwa Kristo pale anapojitoa mwenyewe kwangu?
Katika somo la Injili, Yesu anasema “msipo
ula mwili wake Mwana wa Adamu na kuinywa damu yake hamna uzima ndani yenu”.
Wengi wao walichukizwa na kuanza kuuliza uliza juu ya maneno yake. Inavutia
kwamba wakati Yesu anapokutana na maneno makali ya wengine, anajibu tena kwa
ujasiri mkubwa zaidi na uwazi zaidi. Hili linamuonesha kuwa mtu wa ujasiri
mkubwa, mwenye nguvu na kuelewa. Unafunua pia kwetu sisi ujasiri ambao sisi
tunapaswa kuwa nao katika ulimwengu huu. Ulimwengu tunaoishi ni ulimwengu unao
kataa ukweli. Unakataa ukweli wa maadili, lakini pia unapinga ukweli wa ndani
wa kiroho pia. Ukweli huu wa ndani ni kama uwepo wa uzuri wa Ekaristi Takatifu,
umuhimu wa sala za kila siku, unyenyekevu, na kumtegemea Mungu, kuweka mapenzi
ya Mungu mbele kuliko kitu chochote nk. Tunapaswa kutambua kuwa kila mara
tunapo sogea karibu zaidi na Mungu, ndivyo tunavyozidi kujikabidhi kwake zaidi,
na tutakapo hubiri ukweli wa Mungu ndivyo tunavyo upa ulimwengu shinikizo uache
kutuiba kutoka kwa Mungu.
Sasa tufanye nini? Tunajifunza kutoka katika
ujasiri na nguvu ya Yesu. Tunapojikuta sisi wenyewe tukiwa katika changamoto au
tunapo hisi kana kwamba Imani yetu inashambuliwa, ndivyo tunavyo takiwa tuzame
ndani zaidi na kuwa waaminifu zaidi na zaidi. Hili litatufanya tuwe na nguvu
zaidi na kufanya vishawishi vinayokuja kuwa nafasi ya neema! Chagua kuiga
ujasiri na ushupavu wa Bwana wetu na utakuwa chombo chenye kuonekana cha neema
na huruma.
Sala: Bwana, ninaomba unipe ujasiri wa nguvu
zako . Ninaomba unipe mwangaza katika utume wangu na unisaidie kukutumikia
kiaminifu katika kila kitu. Ninaomba nisiwe muoga ninapo kutana na changamoto
za maisha bali nitazame hamu yangu ya kukutumikia kwa moyo wangu wote. Yesu
nakuamini wewe. Amina.
Copyright ©2013-2024 ©FurKat, Furaha ya
Kikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com
No comments:
Post a Comment