
“KWARESIMA YA UKARIMU”
Tafakari ya Kwaresima
Jumamosi, Aprili, 5, 2025,
Juma la 4 la Kwaresima
Yer 11: 18-20;
Zab 7: 2-3, 9-12;
Yn 7: 40-53.
KUMSIKILIZA YESU
Ni vigumu kutokuitika unapokutana na ujumbe wa Yesu. Baadhi ya
watu waliamini kuwa Yeye ni nabii, wengine kwamba ni Masiha, na hivyo walikuwa
wameshawishika huenda ni mmoja wapo kati ya hao. Lakini muonekano wa wakuu
unashangaza. Walienda kumkamata lakini wakarudi mikono mitupu, kwasababu
hawakuwahi kumsikia yeyote akiongea kama yeye. Mafariyo na Waandishi wanaonekana
kutopendezwa. Muonekano wa Nikodemu unaonekana kuwa ni wa woga. Moyo wake
ulimwambia amlinde Yesu, lakini akili yake ilimwambia asije akajihatarishia
maisha.
Wakati Yesu anafundisha kuna kitu kilichokuwa kikiwakilishwa zaidi
ya maneno yake. Maneno yake yana nguvu ya kufanya mambo upya, lakini ilikuwa ni
kwa jinsi yake ya kuongea. Ni vigumu kuelezea, lakini ni hakika kwamba alivyo
ongea, aliwasilisha pia nguvu, utulivu, hali ya kuguswa na kukubali na pia
uwepo wake. Aliwakilisha uwepo wake wa Kimungu bila dosari. Watu walitambua tu
huyu mtu, Yesu , ni tofauti na wengine wote, na kujikuta wakisikiliza kila neno
lake.
Mungu anawasiliana nasi kwa namna hii. Yesu bado anaongea nasi.
Tunapaswa tu kuwa wasikivu kwa neno lake. Tunapaswa kuwa wasikivu katika njia
ambazo Mungu anaongea nasi katika hali ya wazi kabisa yenye kugusa mioyo yetu,
na kwa mamlaka yake. Inaweza kuwa ni kitu mtu anasema, au matendo anayofanya
mtu yakatugusa. Inaweza kuwa kitabu nilichosoma, au kitu ambacho nasikia katika
maandiko. Katika hali yeyote inavyoweza kuwa, tunapaswa kusikiliza kwani ndipo
tunapokutana na Yesu mwenyewe. Kujikita katika kufuata njia ya Mungu ni
kujitahidi kutokusikiliza vipingamizi na shutuma unazoweza kupata katika
kufuata sauti yake. Sauti yake inapaswa kushinda na kukuvuta katika kufanya
yale yote anayopenda uyafanye.
Sala: Bwana, ninaomba niwe msikivu kwa sauti yako isiyo na dosari
na katika mamlaka unayo zungumza. Na ninapo kusikiliza, Bwana mpendwa, nisaidie
niitike kwa Imani licha ya vipingamizi vya wengine. Yesu, nakuamini wewe.
Amina.
No comments:
Post a Comment