
“KWARESIMA YA UKARIMU”
Tafakari ya Kwaresima
Jumatano, Aprili 16, 2025.
Juma Kuu
Isa 50: 4-9;
Zab 68: 8-10, 21-22, 31, 33-34;
Mt 26: 14-25.
KUBEBA MISALABA YETU!
“Naliwatolea wapigao mgongo wangu, na
wang'oao ndevu mashavu yangu; sikuficha uso wangu usipate fedheha na kutemewa
mate." Mstari huu kutoka kitabu cha nabii Isaya unatukumbusha juu ya
uchungu wa Yesu. Lakini, tunaweza kufikiria tu kile alichokihisi Yesu aliposoma
maneno haya ya Isaya. Je, unafikiri maneno haya yalimpelekea awe na hofu? Au
labda kwa sababu yeye alikuwa mwana wa Mungu, jambo hili halikumsumbua yeye
kabisa? Pangine ukweli upo sehemu fulani kati ya hayo. Kuwa binadamu, Yesu
kiasili alihisi matatizo makubwa juu ya kile kilichokuwa kikimngojea yeye.
Lakini katika Umungu wake, aliweza kutamka kwa kujiamini sana, Bwana Mungu
ndiye msaada wangu hivyo sina mashaka. Hivyo hakika alikuwa na hofu kubwa juu
ya majaribu yaliopo mbele yake, vilevile Yeye alijawa na nguvu akijua kuwa Baba
yake alikuwa pamoja naye na kamwe asinge mwacha.
Kuna uwiano hapa kwa maisha yetu. Hatuwezi
kuona wakati ujao, lakini tunatambua kuwa tuna ugumu fulani waweza kuja katika
maisha yetu na tunapaswa kuushughulikia. Pengine hatupo katika hali ambayo
dhambi yetu inatuonesha tuna mkana Yesu moja kwa moja, lakini kila mmoja
anaweza kuona aina fulani ya dhambi katika maisha yake. Tumia juma hili kwa
uaminifu na kweli. Huruma ya Mungu ni ya ndani sana na njema mno, kiasi kwamba
ungeielewa, kusingekuwa na haja ya kubaki na dhambi zako ukifikiria niungame
namna ghani. Hali halisi haipo kama tunavyo ifikiria sisi wenyewe. Kama Yesu,
tunajikabidhi kwa upendo na msaada wa Baba yetu wa Mbinguni. Tukiwa naye, ni
hakika kwamba tunashinda tatizo lolote lile, kwani hawezi kuwatupa watoto wake.
Sala: Bwana, ninaomba unisadie katika juma
hili niweze kukabili dhambi zangu na udhaifu wangu. Mimi ni mdhambi, Bwana
mpendwa, lakini inaweza kuwa vigumu sana kwangu kukubali ukweli huu. Ninaomba
nikabidhi dhambi zangu kwako, ili niweze kuwa huru, na kupokea nafasi katika
huruma yako kuu. Yesu, nakuamini wewe. Amina.
No comments:
Post a Comment