“KUFUFUKA NA KRISTO”
Tafakari ya Pasaka
Jumapili, Aprili 20, 2025.
Jumapili ya Pasaka
JUMAPILI YA PASAKA
Mdo 10: 34, 37-43
Zab118: 1-2,15-17,22-24
Kol 3: 1-4 or 1Cor 5: 6-8
Yn 20: 1-9
ALLELUIA! YESU AMEFUFUKA KWELI KWELI!
Kwaresima imeisha sasa ni kipindi cha kuadhimisha furaha kuu ya
Pasaka! Ulimwengu unafurahia ushindi wa Kristo juu ya dhambi na mauti. Mungu
kwa upendo wake kamili na hekima yake, aliishinda dhambi na matokeo ya
dhambi(mauti) na kutumia kama njia ya wokovu wa ulimwengu. Kwa kuruhusu dhambi
za dunia zimsulubishe na kuteswa na kufanya mateso hayo na dhambi hiyo kuwa
kielelezo cha kuleta ukombozi. Yesu aliiangamiza dhambi kwa kuangamiza matokeo
ya dhambi ambayo ni mauti. Mauti imepotezwa kwa ufufuko. Ufufuko wa Yesu
unaondoa matokeo yote ya dhambi kwao wote wanaojikita kwake.
Kama mateso makali ya Yesu, Mwana wa Mungu, yanaweza kubadilika na
kuwa tukio kubwa katika historia ya maisha ya Mwanadamu, ndivyo, mateso yako
mwenyewe mizigo yako, hata dhambi zako, zinaweza kuwa chanzo cha furaha yako
kubwa kama utamruhusu Mungu ayabadilishe kwenda kwenye ufufuko.
Pasaka maana yake ni hakuna chochote kinacho weza kutuweka mbali
na furaha ambayo Mungu anataka kutupatia. Tambua kwamba Mungu anapenda ufurahie
furaha ya Pasaka katika maisha yako. Muache yeye akujaze na furaha kuu ambayo
ni ufufuko pekee unaweza kuleta. Mungu anataka Pasaka ianze sasa katika maisha
yako.!
Katika Injili maneno ya Petro yanachanganyika na majuto ya
kumwangusha Yesu. Alisema kwamba atakufa kwa ajili yake, lakini akakimbia.
Sasa, Yesu ni mzima! Wala hakuna hukumu. Yesu ametupatanisha naye, tumekaa naye
katika mkono wa kuume wa Mungu. Tupo huru kutoka katika sheria ya dhambi na
mauti. Tumesamehewa. Maneno tunayosikia kutoka katika maneno ya Petro kama
yalivyo andikwa kwenye kitabu cha matendo ya Mitume, yanatikisa kwa furaha
yote, nguvu na ujasiri kwamba Yesu, ambaye tulimshuhudia akihubiri na kuponya,
tuliye muona akisulubiwa, sasa tumeona kwamba amefufuka, yupo mzima.
Baba Mtakatifu anasema “Kuwa Mkristo sio kwasababu ya matokeo ya
uchaguzi wa sheria za maadili, bali kwasababu ya kukutana na tukio, mtu, ambaye
anatoa maana nyingine katika maisha na muelekeo mzuri” maisha haya ya
kubadilisha hayajawekwa kwasababu ya wachache, bali ni mwaliko wa wote. Kila
Mkristo anaitwa kwenye maisha mapya ya kukutana na Yesu Kristo, au kuacha uwazi
ndani ya moyo na kumruhusu aingie ndani akubadilishe. Katika siku hii ya Pasaka
tusimame imara tukimuomba atufanye wapya kwa kukutana naye. Tutamani kukutana
na wengi ambao hawajaona, lakini wakaamini, kwasababu wamesikia. Tuwe mashahidi
wa ufufuko.
Sala: Bwana, ninakuomba nikufanye wewe ubadilishe kila msalaba
katika maisha yangu kwenda kwenye furaha Kuu. Bwana, ninaomba furaha yako ijaze
maisha yangu na kunijaza nguvu kwa kila kitu. Yesu, nakuamini wewe. Amina

No comments:
Post a Comment