“ASALI ITOKAYO MWAMBANI”
Tafakari ya kila siku
Jumatatu, Mei 27, 2024.
Juma la 8 la Mwaka wa Kanisa
1 Pet 1: 3-9;
Zab 111: 1-2,5-6,9-10;
Mk 10: 17-27
KUJIBU WITO WA YESU!
Katika Injili ya leo, Yesu anamuangalia “kijana tajiri” na
“anampenda”. Yesu anamwitia kuachia kila kitu alicho nacho, kutoa yote na
kumfuata yeye. Yesu alimwalika afanye hivi kwasababu ya upendo. Yesu anamwita
huyu kijana ili aweze kupata mengi zaidi kuliko yale aliokuwa nayo. Ndio maana
Yesu alimtazama kwa mapendo kabla hajamwita huyu kumfuata katika hali ya kuacha
yote kabisa. Lakini katika hali hii ya huyu Yesu anayependa inaumiza. Ilikuwa
inaumiza katika hali kwamba kumfuata huyu Yesu ilihitaji sadaka ya kila kitu.
Ilikuwa ni kujikana na kuachia yote. Ilikuwa ni ngumu katika hali ya kibinadamu
na hali ya kidunia. Lakini upendo wa Yesu kwa huyu kijana ulikuwa kamili kiasi
kwamba ulikuwa umsaidie huyu kijana kuachia yote na kupata mengi zaidi. Lakini
kama ilivyo kawaida kwa Mungu, anapenda kumpa mwanadamu uhuru achague mwenyewe
ka uhuru wake kamili.
Tunaitwa kufanya hivyo pia. Tunaweza tusiitwe kumfuata Yesu katika
hali ya kuacha yote katika hali ya mali tulionayo. Lakini tunaitwa katika hali
ya kumfuata Yesu katika hali ya kumwamini hakika na kujikabidhi kwenye mapenzi
yake. Na kwa njia ya mapenzi yake haiwezekani bila sadaka. Sadaka katika hali
ya juu.
Majibu yetu ya jinsi ya kufuata wito wa Yesu ni muhimu. Ni namna
ghani tunaitikia wito huu wa Yesu na kujitoa kabisa kwake? Huyu kijana tajiri
alijibu kwanza kwa huzuni. Hakukubali wito aliomwitia Yesu. Mara nyingi hali
hii imekuwa majibu yetu. Tunataka kumfuata Yesu katika hali ya uaminifu bila
kujali anatuamuru nini. Lakini tunapopewa hali halisi ya kujibu wito wake,
tunarudi nyuma kwa huzuni kwakufikiria wito huo unagharimu mno.
Tuangalie, angalia maisha yako binafsi na angalia ni kwa jinsi
ghani ulivyo tayari kusema “ndio” kuachia vyote kwa jinsi Yesu atakavyo
kuambia. Kwa kusema “ndio” katika hali ya sadaka ni uamuzi mzuri kabisa ambao
unaweza kufanya. Katika hali ya kweli, ni uamuzi wa kweli uliokubalika wa hali
ya utukufu ambao mtu anaweza kuishi.
Sala: Bwana, kukufuata wewe inawezekana ikaonekana kuwa ngumu na
kugharimu. Inawezekana kuwa kama inazidi mno. Nisaidie hasa katika hali hizi,
nikuamini wewe zaidi ya yale yote nilio nayo katika ulimwengu huu. Yesu,
nakuamini wewe. Amina
Copyright
©2013-2024 ©FurKat, Furaha ya Kikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com
No comments:
Post a Comment