“ASALI ITOKAYO MWAMBANI”
Tafakari ya kila siku
Alhamisi, Novemba 14, 2024
Juma la 32 la Mwaka wa Kanisa
Flm1:7-20;
Zab 145:7-10;
Lk 17:20-25
UFALME WA MUNGU UPO KATI YETU.
Barua ya Mt. Paulo kwa Filemoni, ni barua fupi sana, ina aya tu, lakini ni barua ilioandikwa kwa utaalamu mkubwa. Mt. Paulo anaianza kwa kukiri uzuri wa Filemoni na kwa jinsi alivyo wawekea na kuwaonesha wema jumuiya ya Kikristo. Mt. Paulo anasisitiza juu ya Onesimo, ambaye alikuwa mtumwa wa Filemoni, na anamuomba amchukue Onesimo kama ndugu katika Kristo. Na anamuomba Filemoni amsamehe Onesimo kwa kosa lolote alilotenda kabla. Unaweza kuona ni kwa jinsi ghani Ufalme wa Mungu ulivyowekwa wazi na Paulo. Ufalme wa Mungu ambao upo wazi kwa kila mtu. Kazi yetu ni kuutambua ufalme huo ndani yetu.
Tunapokuwa tayari kutangaza msamaha tunakuwa tunaonesha tunu za ufalme wa Mungu tungali hapa duniani. Kushindwa kusamehe na kubeba watu moyoni pengine limekuwa tatizo la wengi. Leo nasi tunaalikwa tusiwabebe watu na wala tusikubali kujiumiza wenyewe kwa kubeba chuki kwani chuki ni sumu ndani wa mwili wa mtu mwenyewe.
Sala: Bwana Yesu nisaidie mimi niweze kueneza Ufalme wako kwa njia ya maneno na matendo yangu.
Copyright ©2013-2024 ©FurKat, Furaha ya Kikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com
No comments:
Post a Comment