“MBEGU ZA UZIMA”
Tafakari ya kila Jumapili
Oktoba 27, 2024
Dominika ya 30 ya Mwaka
Yer 31: 7-9;
Zab 126: 1-6 (K) 3;
Ebr 5: 1-6;
Mk 10: 46-52
HAMU YAKUUONA WOKOVU WETU–YESU!
Somo la kwanza kutoka Kitabu cha Nabii Yeremia, kinaonesha upendo wa Mungu kwa wanadamu. Mungu anajulisha mipango yake ya kumkomboa mwanadamu. Anapanga kuwakusanya wote pamoja, kutoka pande zote za dunia, kama Wagonjwa, Vipofu, Viwete, Yatima na Wajane; hataki kumwacha yeyote kwasababu ya upendo wake wa kuokoa.Na hii ndio sababu, lazima kuwe na furaha kuimba na kushangilia, kwasababu Mungu anatuchukua sisi kama watoto wake na anatupa upendeleo wakumuita yeye Baba yetu. Ahadi hii ilikuwa ni tumaini kubwa kwa wana waisraeli kwani baada ya utumwa wa Babeli walitapakaa katika nchi mbali mbali. Munngu anatoa matumaini ya kuwakusanya tena kama Wanae.
Katika somo la Injili leo, tunaona Imani ya kipofu Batimayo aliyekuwa akisubiri wakati wa wokovu. Alikaa pembezoni mwa barabara akiomba. Watu wengi walikuwa wakitembea wakisafiri pamoja na Yesu na walimkaribia Batimayo. Yesu inawezekana alimuona Batimayo au kwasababu ya watu wengi,hakuweza kumuona . Batimayo anawasikia na anaanza kujongea kumfuata Yesu. Ana mtambulisha Yesu kama “Mwana wa Daudi” [ jina la Masiha ambaye angekuja] akimtambua Yesu kuwa Masiha-Kristo. Umati wa watu walimzuia wakimnyamazisha Batimayo, lakini yeye alipaaza sauti zaidi akiomba msaada. Lakini Yesu alikisikia kilio chake cha uchungu, na anasema “Mwiteni”. Wanamleta kwa Yesu. Kinachofuata ni kuponywa. Yesu anamwambia “Nenda Imani yako imekuponya”. Na mara anaweza kuona tena na Batimayo anafuatana nao wakitembea barabarani.
Katika mtazamo wetu wa sasa, sisi pia tupo kama yule kipofu, umati unaharibu, hisia, marafiki, kazi n.k, vinavyo tufunga tushindwe kumfikia Yesu vizuri. Tunamsikia Yesu akipita karibu nasi, kwa Injili tunayo isikia Kanisani, katika nyimbo mbali mbali za dini, nyingine tunazo pokea kupitia Facebook, Whatsapp,n.k je tunawashirikisha na wengine au tunawazuia kama ule umati? Tujaribu kufikiria ni mara ngapi Yesu ametupita kwasababu hatumuiti na kumlilia kwa mahitaji yetu. Je unataka kubakia bila kupata upendo wa Yesu? Yesu anatusubiri tumuite.
Marko, katika Injili, anaonesha kwamba tendo hili lilitokea wakati Yesu na umati wa watu walipokuwa wanauacha mji [Mk 10:46 ].Ni mawazo mazuri ingawaje Yesu alikua njiani kuelekea Yerusalemu kuteswa, alipata muda wakusimama na kumuita Batimayo, na kumuuliza alitaka nini kutoka kwake. Chochote alicho fundisha wakati akitembea, vilisahaulika kwa kwasababu ya mahitaji ya watu. Usije ukafikiria hata siku moja ya kwamba Yesu hana muda na hitaji lako. Koti lilitupwa pembeni. Hakuwa na jambo lingine laku hangaikia koti lake. Koti, pengine linawa kilisha maisha yake ya zamani, na sasa Yesu ndiye maisha yake mapya.
Kwasababu alikuwa kipofu, watu walimuongoza kwenda kwa Yesu. Lilikuwa jambo nzuri kuhusu hitaji lake, kwanini Yesu alimuuliza alitaka nini kwake? Maisha yake yalikuwa tegemezi sana kwa wengine kwahiyo yalibadilika kwasababu aliponywa. Watu bado wangefikiria kipindi chake akiwa anaomba kabla ya kuponywa. Hangehitaji tena kuomba, je ni jambo hilo alilolitaka kweli? Mara nyingi Yesu anatutaka tuweke katika maneno dhahiri tunaihitaji nini kwake. Anatazama aweze kuona ni kwa jinsi gani mioyo yetu inaendana na kile tunachotaka afanye kwetu. Ninaogopa ninachokiomba hakijibiwi kwasababu sina uvumilivu. Moyo wangu lazima uwe na kile nikiombacho. Vipi kuhusu hali yako binafsi? Ni mara ngapi unaingia ndani ya maisha yako ya sala? Moyo wa Batimayo ulikuwa ndani yakile alichokiomba kwa Kristu. Ulijawa na nguvu na shauku. Uwezo wake wakuita bila kukatizwa na sauti za watu au vitu ni muhimu sana katika maisha ya sala iliyo ya kweli. Yesu anamkuta mtu huyu akiwa katika hitaji kubwa na asingeweza kumpita tuu.
Batimayo hakuwa amewahi kumuona Yesu, alichojifunza kuhusu Yesu ilikuwa tuu yale aliyo simuliwa na wengine. Wakati watu walipo mwambia “jipe moyo! Simama anakuita”(Mk 10:49), aliamini ushuhuda wao, akatupa koti lake wakamuongoza kwenda kwa Kristo.Je, unaweza kumuona Yesu pia kwa jicho la Imani? Alichofanya kwa Batimayo anaweza kufanya pia kwako. Yesu alipomaliza kusema maneno “upate kuona, Imani yako imekuponya” macho ya kipofu yalifunguka akaweza kumuona…Mkombozi wa Ulimwengu, Yesu, yupo tayari kufungua upofu wetu pia. Tupo tayari kupokea na kukaa katika upendo wake na utukufu wake? Tusilisikie neno lake na kutupa koti la dhambi zetu na kumfuata.
Sala: Bwana, fungua macho ya moyo wangu. Nataka kukuona. Amina.
Copyright ©2013-2024 ©FurKat, Furaha ya Kikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com
No comments:
Post a Comment