“MBEGU ZA UZIMA”
Julai 21, 2024
Dominika ya 16 ya Mwaka
Yer 23:1-6;
Zab 23 (K) 1;
Efe 2:13-18;
Mk 6:30-34.
KAMA KONDOO WASIO NA MCHUNGAJI !
Wakati Yesu na wanafunzi wake walipoenda mahali
pa faragha kwa ajili ya kupumzika, watu walienda mbio huko kumsikiliza na
kupata Baraka. Makutano waliwaendea faraghani, lakini Kristo hakuwalaumu;
waliingia bila kukaribishwa wala kutakiwa kwenye pumziko lao walilolistahili,
lakini Yesu hakupatwa na uchungu wowote.Badala yake aliwaonea huruma akisema
kwamba walikuwa kama kondoo wasio na mchungaji. Ilikuwa ni umati wa watu,
ambaowalikuwa na hamu ya kufundishwa, lakini hapakuwa na mtu wa kuwafundisha; walihitaji
kulishwa na mafundisho mazuri, lakini hapakuwa na wakuwalisha. Kwa hiyo,
Alikuwa na huruma juu yao, na hakuwafundisha tu, pia aliwaponya waliokuwa
wagonjwa.
Katika somo la kwanza nabii Yeremia anaonesha
kasoro za wachungaji wa taifa la Mungu katika Agano la Kale. Katika nabii
Yerernia, Mungu anakemea tabia mbaya za viongozi wa Israeli zilizopelekea taifa
zima la Mungu kuangamia kwa kupelekwa utumwani katika uchi ya Babeli. Mungu
anaahidi kuchipusha chipukizi la haki kutoka shina la Daudi, atakayemiliki
ufalme na kutenda kwa haki. Utabiri huu unatimia katika Yesu Kristo aliye
mchungaji mwema wa kundi lake
Yesu Kristo ni Mchungaji Mwema. Viongozi wa
Agano la Kale walitambua na kujiona kuwa wamechaguliwa na Mungu kuliongoza
taifa a Israeli, lakini walishindwa kutimiza wajibu wao ipasavyo. Kristo Yesu
ni Mchungaji ya hakika. Alianza kuhubiri na kukusanya taifa la Mungu,
amewagawia Mwili na Damu yake (Ekaristi Takatifu) na Neno lake, yaani
mafundisho yake kwa watu wote
Katika maisha yetu na katika sehemu mbalimbali
kama vile: familia, jumuiya, serikali, kanisa n.k. viongozi na watu wale
wanapaswa kuiga mfumo wa Yesu. Tunakumbushwa tena leo wachungaji lazima wawe na
upendo, huruma, upole, uvumilivu na unyenyekevu katika shughuli zao. Tukiwa tayari
wafuasi wa Kristo tuwe na roho ya huruma kwa wengine.
Sala: Bwana, Tusaidie kuwa viongozi vema kufuata
mfano yako. Amina!
No comments:
Post a Comment