MASOMO
YA MISA JUMAPILI, JULAI 21, 2024
Dominika
ya 16 ya mwaka B
Somo
la 1
Yeremia:23:
1 - 6
Ole
wao wachungaji, wanaoharibu kondoo za malisho yangu na kuwatawanya! Asema
Bwana.
Kwa
sababu hiyo Bwana, Mungu wa Israeli, asema hivi, juu ya wachungaji wanaowalisha
watu wangu, Mmetawanya kundi langu, na kuwafukuza, wala hamkwenda kuwatazama;
angalieni, nitawapatiliza uovu wa matendo yenu, asema Bwana.
Nami
nitakusanya mabaki ya kundi langu, katika nchi zile zote nilizowafukuza, nami
nitawaleta tena mazizini mwao; nao watazaa na kuongezeka.
Nami
nitaweka juu yao wachungaji watakaowalisha; wala hawataona hofu tena, wala
kufadhaika, wala hatapotea hata mmoja wao, asema Bwana.
Tazama
siku zinakuja, asema Bwana, nitakapomchipushia Daudi Chipukizi la haki; naye
atamiliki mfalme, atatenda kwa hekima, naye atafanya hukumu na haki katika
nchi.
Katika
siku zake Yuda ataokolewa, na Israeli atakaa salama, na jina lake atakaloitwa
ni hili, Bwana ni haki yetu.
Wimbo wa katikati
Zaburi:23.
Bwana ndiye mchungaji wangu, Sitapungukiwa na kitu.
Katika
malisho ya majani mabichi hunilaza,
Kando ya maji ya utulivu huniongoza.
Kando ya maji ya utulivu huniongoza.
Hunihuisha
nafsi yangu;
(K)
Bwana ndiye mchungaji wangu, sitapungukiwa na kitu.
Huniongoza Katika njia za haki kwa ajili ya
jina lake,
Naam,
nijapopita kati ya bonde la uvuli wa mauti,
Sitaogopa mabaya; Kwa maana Wewe upo pamoja nami,
Gongo lako na fimbo yako vyanifariji.(K)
Sitaogopa mabaya; Kwa maana Wewe upo pamoja nami,
Gongo lako na fimbo yako vyanifariji.(K)
Waandaa meza mbele yangu,
Machoni pa watesi wangu.
Umenipaka mafuta kichwani pangu,
Na kikombe changu kinafurika. (K)
Machoni pa watesi wangu.
Umenipaka mafuta kichwani pangu,
Na kikombe changu kinafurika. (K)
Hakika wema na fadhili zitanifuata
Siku zote za maisha yangu;
Nami nitakaa
nyumbani mwa Bwana milele.(K)
Somo la 2
Waefeso
2:13 - 18
Katika
Kristo Yesu, ninyi mliokuwa mbali hapo kwanza mmekuwa karibu kwa damu yake
Kristo.
Kwa
maana yeye ndiye amani yetu, aliyetufanya sisi sote tuliokuwa wawili kuwa
mmoja; akakibomoa kiambaza cha kati kilichotutenga.
Naye
akiisha kuuondoa ule uadui kwa mwili wake; ndiyo sheria ya amri zilizo katika
maagizo; ili afanye hao wawili kuwa mtu mpya mmoja ndani ya nafsi yake;
akafanya amani.
Akawapatanisha
wote wawili na Mungu katika mwili mmoja, kwa njia ya msalaba, akiisha kuufisha
ule uadui kwa huo msalaba.
Akaja
akahubiri amani kwenu ninyi mliokuwa mbali, na amani kwao wale waliokuwa
karibu.
Kwa
maana kwa yeye sisi sote tumepata njia ya kumkaribia Baba katika Roho mmoja.
Shangilio:
Yohana:15.15
Aleluya aleluya!
Siwaiti
tena watumwa; kwa maana mtumwa hajui atendalo bwana wake; lakini ninyi
nimewaita rafiki; kwa kuwa yote niliyoyasikia kwa Baba yangu nimewaarifu.
Aleluya.
Injili.
Marko
6: 30 - 34
Mitume
walikusanyika mbele ya Yesu; wakampa habari za mambo yote waliyoyafanya, na
mambo yote waliyoyafundisha.
Akawaambia,
Njoni ninyi peke yenu kwa faragha, mahali pasipokuwa na watu, mkapumzike
kidogo. Kwa sababu walikuwako watu wengi, wakija, wakienda, hata haikuwapo
nafasi ya kula.
Wakaenda
zao faragha mashuani, mahali pasipokuwa na watu.
Watu
wakawaona wakienda zao, na wengi wakatambua, wakaenda huko mbio kwa miguu, toka
miji yote, wakatangulia kufika.
Naye
aliposhuka mashuani, akaona mkutano mkuu, akawahurumia; kwa sababu walikuwa
kama kondoo wasio na mchungaji; akaanza kuwafundisha mambo mengi.
Neno
la Bwana.....Sifa kwako Ee Kristo.
Copyright
© 2024, "MASOMO YA MISA" published by T.M.P. Book Department, Tabora
– Tanzania. Readings reproduced by Furaha ya Kikatoliki: see
www.fur-kat.blogspot.com
No comments:
Post a Comment