MASOMO
YA MISA, JULAI 16, 2024
JUMANNE
YA 15 YA MWAKA
SOMO
1
Isa.
7: 1 – 9
Ilikuwa
katika siku za Ahazi, mwana wa Yothamu, mwana wa Uzia, mfalme wa Yuda, Resini ,
mfalme wa Shamu, na Peka, mwana wa Remalia, mfalme wa Israeli, wakapanda
wakaenda Yerusalemu ili kupigana nao, lakini hawakuweza kuushinda. Kisha watu
wa nyumba ya Daudi wakaambiwa kwamba Shamu wamefanya mapatano na Efraimu. Na
moyo wake ukataharuki, na moyo wa watu wake, kama miti ya mwituni itikiswavyo
na upepo.
Basi
Bwana akamwambia Isaya, Haya, toka, umlaki Ahazi, wewe na Shear-yashubu mwana
wako, huko mwisho wa mfareji wa birika la juu, katika njia kuu ya uwanja wad
obi; ukawaambie, Angalia, ukatulie; usiogope wala usife moyo, kwa sababu ya
mikia hii miwili ya vinga hivi vitokavyo moshi; kwa sababu ya hasira kali ya
Resini na Shamu, na mwana wa Remalia. Kwa kuwa Sahmu amekusudia mabaya juu
yako, pamoja na Efraimu na mwana wa Remalia, wakisema, Haya, na tupande ili
kupigana na Yuda na kuwasumbua, tukabomoe mahali tupate kuingia, na
kummilikisha mfalme ndani yake, huyo mwana wa Tabeeli.
Bwana
Mungu asema hivi, Neno hili halitasimama wala halitakuwa. Kwa maana kichwa cha
Shamu ni Dameski, na kichwa cha Dameski ni REsini; na katika muda wa miaka
sitini na mitano Efraimu atavunjika vipande vipande, asiwe kabila ya watu tena;
tena kichwa cha Efraimu ni Samaria, na kichwa cha Samaria ni mwana wa Remalia.
Kwamba hamtaki kusadiki, bila shaka hamtathibitika.
Neno
la Bwana… Tumshukuru Mungu.
WIMBO
WA KATIKATI
Zab.
48: 1 – 7 (K) 8
(K)
Mji wa mungu wetu ataufanya imara hata milele.
Bwana
ndiye aliye mkuu,
Na
mwenye kusifiwa sana.
Katika
mji wa Mungu wetu,
Katika
mlima wake mtakatifu.
Kuinuka
kwake ni mzuri sana,
Ni
furaha ya dunia yote. (K)
Mlima
Sayuni pande za kaskazini,
Mji
wa Mfalme mkuu.
Mungu
katika majumba yake
Amejijulisha
kuwa ngome. (K)
Maana,
tazama, wafalme walikusanyika;
Walipita
wote pamoja.
Waliona,
mara wakashangaa;
Wakafadhaika
na kukimbia. (K)
Papo
hapo tetemeko liliwashika,
Utungu
kama wa mwanamke azaaye.
Kwa
upepo wa mashariki
Wavunja
jahazi za Tarshishi. (K)
SHANGILIO
Zab.
119: 34
Aleluya,
aleluya,
Unifahamishe
name nitaishika sharia yako, nitaitii kwa moyo wangu wote.
Aleluya.
INJILI
Mt.
11:20 – 24
Yesu
alianza kuikemea miji ile ambamo ndani yake ilifanyika miujiza yake iliyo
mingi, kwa sababu haikutubu.
Ole
wako, Korazini! Ole wako, Bethsaida! Kwa kuwa kama miujiza iliyofanyika kwenu
ingalifanyika katika Tiro na Sidoni, wangalitubu zamani kwa kuvaa magunia na
majivu. Walakini nawaambieni, itakuwa rahisi Tiro na Sidoni kustahimili adhabu
zao siku ya hukumu kuliko ninyi.
Nawe
Kapernaumu, je! Utakuzwa mpaka mbinguni? Utashushwa mpaka kuzimu; kwa kuwa kama
miujiza iliyofanyika kwako ingalifanyika katika Sodoma, ungalikuwapo mji huo
hata leo. Walakini nawaambieni, itakuwa rahisi nchi ya Sodoma kustahimili
adhabu yake siku ya hukumu kuliko wewe.
Neno
la Bwana… Sifa kwako Ee Kristo.
Copyright
© 2024. Readings reproduced by Furaha ya Kikatoliki: see
www.fur-kat.blogspot.com
No comments:
Post a Comment