"ASALI ITOKAYO MWAMBANI"
Tafakari ya kila siku
Jumanne, Julai 16, 2024
Juma la 15 la Mwaka
Isa. 7: 1 – 9
Zab. 48: 1 – 7 (K) 8
Mt 11:20-24
AMKA NA UITIKE WITO!
Katika somo la Injili Yesu anaongea na watu wa mji ambao amefanya miujiza
mingi na uponyaji, lakini watu wanaendelea na mambo yao ya kawaida kama vile
hakuna kitu kinacho tokea kati yao. Yesu anawaambia waamke na kutubu!
Wanachagua wenyewe kuteseka milele na maangamizi. Sidhani kama kuna mmoja wetu
anaweza kutamani kuchagua jambo kama hilo kuteseka milele au mtu mwingine
ateseke milele. Yesu yupo hapa, yupo nasi leo, tunapaswa kujikita katika ukweli
huu. Tunapaswa kumgeukia yeye, na kumwambia utusamehe kwa yale yote ambayo
tumekutendea, na hivyo kukabidhi maisha yetu kwake.
Yesu anawakemea watu wa Korazini na Betsaida kwasababu anawapenda anaona
wanabaki tu katika maisha yao ya dhambi ingawaje ameleta habari njema na
miujiza mingi mikubwa. Walibaki katika hali ya usumbufu, mtegoni,
kuchanganyikiwa, kukataa kutubu, na hali ya kutokuwa tayari kubadilisha njia
zao za maisha. Yesu anaonesha hali ya huruma ya hali ya juu. Yesu anawaonya.
Yesu anawaonya katika hali ya upendo na kutaka wabadilike. Hawakubadillika mara
moja baada ya yeye kuwaalika kwa kufanya miujiza mingi, hivyo alipenda
kubadilisha hali na kuleta hali mpya. Tafakari leo, kama unataka Yesu akuongoze
kwa mapendo utoke katika hali yako , kama unapenda kukubali Injili ya upendo
izame ndani yako.
Kwa wakarmeli, leo ni Sherehe ya Bikira Maria Mlima wa Karmeli. Mama Maria ni namna ya pekee ni mfano wa kuigwa katika maisha ya ukimya, sala ya ndani, kama vile alivyoweka na kutafakari mambo yote moyoni mwake na kudumu katika sala akiwa na mitume. Skapulari ni alama ya ukumbusho wa Upendo wa pekee wa Maria kwetu sisi na pia upendo tulio nao kwake. Ni ukumbusho wa uwepo wake kwetu daima katika maisha yetu na upendeleo wake kwetu. Hakika yeye ni mama na dada pia, akitulinda na kutuongoza kwa mwanae, ambaye, kweye, twapata wokovu. Yupo nasi tunapoishi na tunapokufa. Uvaaji wa skapulari ni alama ya nje ya ukumbusho wa kile ambacho kinaendelea kutokea ndani mwetu. Mama Maria anaonekana wazi kuwa mfano bora wa kile tunachomaanisha, kumfuta Kristo. Maana ya skapulari leo hii, kuvaa vazi la Mama yetu wa Mlima Karmeli, kuvaa pia fadhila zake na kufungua mioyo yetu kwa mwaliko wa Yesu.
Sala: Bwana, nisaidie mimi niweze kuungama dhambi zangu daima. Nisaidie
niweze kuwa chombo cha kuwafanya wenzagu wakurudie. Ninaomba nipokee siku zote
neno lako kwa upendo na kulishirikisha kwa upendo katika hali inayo faa. Yesu,
nakuamini wewe. Amina.
No comments:
Post a Comment