MASOMO YA MISA, JULAI 15, 2024
JUMATATU, JUMA LA 15 LA MWAKA
KUMBUKUMBU YA MT. BONAVENTURE
SOMO 1
Isa. 1:10 – 17
Lisikieni neno la Bwana, enyi waamuzi wa Sodoma; tegeni masikio msikie sharia ya Mungu wetu, enyi watu wa Gomora. Huu wingi wa sadaka zenu mnazonitolea una faida gani? Asema Bwana. Nimejaa mafuta ya kafara za kondoo waume, na mafuta ya kafara za kondoo waume, na mafuta ya wanyama walionona; name siifurahi damu ya ng’ombe wala ya wanakondoo wala ya mbuzi waume. Mjapo ili kuonekana mbele zangu, ni nani aliyetaka neno hili mikononi mwenu, kuzikanyaga aliyetaka neno hili mikononi mwenu, kuzikanyaga nyua zangu?
Msilete tena matoleo ya ubatili; uvumba ni chukizo kwangu; mwezi mpya na sabato, kuita makutano; siyawezi maovu hayo na makutano ya ibada. Sikukuu zenu za mwezi mpya na karama zenu za mwezi mpya na karama zenu zilizoamriwa, nafsi yangu yazichukia; mambo haya yanilemea; nimechoka kuyachukua.
Nanyi mkunjuapo mikono yenu, nitaficha macho yangu nisiwaone; naam, mwombapo maombi mengu, sitasikia; mikono yenu imejaa damu.
Jiosheni, jitakaseni; ondoeni uovu wa matendo yenu usiwe mbele za macho yangu; achene kutenda mabaya; jifunzeni kutenda mema; takeni hukumu na haki; wasaidieni walioonewa; mpatieni yatima haki yake; mteteeni mjane.
Neno la Bwana… Tumshukuru Mungu.
WIMBO WA KATIKATI
Zab. 50: 8 – 9, 16 – 17, 21, 23 (K) 23
(K) Nitamwonyesha wokovu wa Mungu.
Sitakukemea kwa ajili ya dhabihu zako,
Na kafara zako ziko mbele zangu daima.
Sitatwaa ng’ombe katika nyumba yako,
Wala beberu katika mazizi yako. (K)
Una nini wewe kuitangaza sharia yangu,
Na kuliweka agano langu kinywani mwako?
Maana wewe umechukia maonyo,
Na kuyatupa maneno yangu nyuma yako. (K)
Ndivyo ulivyofanya, name nikanyamaza,
Ukadhani ya kuwa Misri ni kama wewe.
Atoaye ya kuwa Misri ni kama wewe.
Atoaye dhabihu za kushukuru ndiye anayenitukuza.
Nitamwonyeshsa wokovu wa Mungu. (K)
SHANGILIO
Aleluya, aleluya,
Ee Bwana unijulishe njia zako, unifundishe mapito yako.
Aleluya.
INJILI
Mt 10: 34 - 11: 1.
Yesu aliwafundisha mitume wake: Msidhani ya kuwa nimekuja kuleta Amani duniani; la! Sikuja kuleta Amani, bali upanga. Kwa maana nalikuja kumfitini mtu na babaye, nab inti na mamaye, na mkwe na mkwe mtu; na adui za mtu ni wale wa nyumbani mwake.
Apendaye baba au mama kuliko mimi, hanistahili; wala apendaye mwana au binti kuliko mimi, hanistahili. Wala mtu asiyechukua msalaba wake akanifuata, hanistahili. Mwenye kuiona nafsi yake ataipoteza; naye mwenye kuipoteza nafsi yake kwa ajili yangu ataiona.
Awapokeaye ninyi, anipokea mimi; naye anipokeaye mimi, ampokea yeye aliyenituma. Ampokeaye nabii kwa kuwa ni nabii, atapata thawabu ya nabii; naye ampokeaye mwenye haki kwa kuwa ni mwenye haki, atapata thawabu ya mwenye haki. Na mtu awaye yote atakayemnywesha mmojawapo wa wadogo hawa ngaa kikombe cha maji ya baridi, kwa kuwa ni mwanafunzi, amin, nawaambia, haitampotea kamwe thawabu yake.
Ikawa Yesu alipokwisha kuwaagiza wanafunzi wake kumi na wawili, alitoka huko kwenda kufundisha na kuhubiri katika miji yao.
Neno la Bwana… Sifa kwako Ee Kristo.
Copyright © 2024. Readings reproduced by Furaha ya Kikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com
No comments:
Post a Comment