Everyday Saint / Maisha ya Watakatifu

VYOMBO VYA UPENDO!



“ASALI ITOKAYO MWAMBANI”
Jumanne, Mei, 14, 2024, 
Juma la 7 la Pasaka

Sikukuu ya Mtakatifu Matia, Mtume

Mdo 1: 15-17, 20-26;
Zab,113: 1-8 (k.8);
Yn 15: 9-17.


VYOMBO VYA UPENDO!

“Hakuna upendo uliyo mkuu kuliko huu, wa mtu kuutoa uhai wake kwaajli ya rafiki zake”. Upendo wa Yesu ni wa pekee na unajifunua kwa majitoleo yake pale msalabani. Upendo wa Yesu ni sadaka na hauna masharti. Yuda hakuutambua upendo huo, lakini sisi tunaitwa kuutambua kama wafuasi wa Kristo.

Kuwa mfuasi wa Kristo kuna mambo matatu yanayo jitokeza katika Injili ya leo, kwanza kabisa, kila Mkristu ana wito wa pekee wakupendana na mwezake. Na pili kila Mkristu ana wajibu wakumfuata Kristo na kutembea katika njia yake ya utakatifu na upendo. Na mwisho kabisa kila Mkristo anapaswa kujiunga na Mungu daima kwa njia ya sala. 

Tumuombe mtakatifu Matia mtume tunae muadhimisha leo atuombee kwa Mungu tuweze kuyashika hayo kama yeye alivyofanikiwa kuyashika kama mtume wa Kristo aliyechukuwa ile nafasi ya Yuda Iskariote.

Sala: Yesu, naomba unisaidie mimi niweze kuwa chombo cha upendo kama mtakatifu Matia mtume. Amina.

Copyright ©2013-2024 ©FurKat, Furaha ya Kikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com

No comments:

Post a Comment